• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 4:50 PM
Hatimaye Moraa awabwaga wapinzani Poland

Hatimaye Moraa awabwaga wapinzani Poland

Na GEOFFREY ANENE

BAADA ya kumaliza mbio za kilomita 21 za Gdynia Half Marathon katika nafasi ya pili mara mbili nchini Poland, Christine Moraa Oigo hatimaye amepata ushindi katika jaribio lake la tatu Jumapili.

Oigo, ambaye alizaliwa Aprili 5 mwaka 1986, alipigiwa upatu kutwaa ubingwa wa Gdynia baada ya kubisha hodi mwaka 2016 na 2017 na pia kushinda Podgorica Half Marathon nchini humo mwaka 2017.

Amenyakua taji la Gdynia kwa saa 1:13:54, sekunde 0.04 nyuma ya Mkenya mwenzake Ruth Matebo (1:13:58) naye Muethiopia Meseret Merine Gezahegn akaridhika katika nafasi ya tatu (1:14:07).

Mkenya Hillary Maiyo, ambaye alilenga kutetea taji, alimaliza katika nafasi ya tano. Mganda Ben Somikwo alitawazwa bingwa mpya kwa saa 1:03:32.

Mhispania El Hassan Oubaddi alikamilisha katika nafasi ya pili sekunde moja nyuma, huku Mkenya Joseph Mumo (1:03:53) akifunga tatu-bora. Muethiopia Mengistu Zelalem, ambaye alimaliza mwaka 2017 katika nafasi ya pili, aliridhika katika nafasi ya nne mwaka huu.

Matokeo (Machi 18, 2018):

Wanaume

Ben Somikwo (Uganda) saa 1:03:32

El Hassan Oubaddi (Uhispania) 1:03:33

Joseph Mumo (Kenya) 1:03:53

Mengistu Zelalem (Ethiopia) 1:04:01

Hilary Maiyo (Kenya) 1:04:04

Marcin Chabowski (Poland) 1:04:53

Wanawake

Christine Moraa Oigo (Kenya) saa 1:13:54

Ruth Matebo (Kenya) 1:13:58

Meseret Merine Gezahegn (Ethiopia) 1:14:07

Viktoriya Khapilina (Ukraine) 1:14:19

Agnieszka Gortel (Poland) 1:16:31

Monika Kaczmarek (Poland) 1:16:57

You can share this post!

Wakenya watwaa dhahabu Mbio za Nyika Algeria

Shujaa kupigania ubingwa kwenye Victoria Falls Sevens

adminleo