Michezo

Daniel Sturridge apigwa marufuku, atakiwa asicheze kandanda kwa muda wa wiki mbili

July 19th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MASHIRIKA na CECIL ODONGO

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge amepigwa marufuku kucheza kabumbu kwa muda wa wiki mbili na pia kutozwa faini ya Sh9,630,500 milioni kwa kupatikana na hatia ya kukiuka kanuni zinazowaongoza wachezaji kuhusu mchezo wa kamari.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza ‘The Three Lions’ awali alipigwa marufuku ya wiki sita lakini ikapunguzwa hadi mbili na sasa atakuwa huru kucheza soka baada ya Julai 30, 2019.

Mnamo Novemba , 2018, Sturridge alikabiliwa na makosa 11 yanayokiuka kanuni za mchezo wa soka, tisa kati ya hayo ikiwa ni kupuuza sheria za Shirikisho la Soka Nchini Uingereza(FA) kuhusu ‘kuweka siri habari za ndani za shirikisho’

FA hata hivyo imesema kwamba itawasilisha rufaa dhidi ya tume huru ya uchunguzi iliyomwondolea Sturridge baadhi ya makosa hayo, ikidai kwamba alitoa habari za siri kuhusu uhamisho wake wa kujiunga na Sevilla uliofaa kufanyika Januari, 2018.

Sturridge alimweleza mwanafamilia wake kubashiri kwamba angehamia Sevilla.