• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Karugwa yapania makubwa raundi hii

Karugwa yapania makubwa raundi hii

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Karugwa Girls ya Meru inapania kujituma kiume kwenye fainali za kitaifa za soka la mashindano ya Shule za Upili muhula wa pili ili kuibuka kati ya tatu bora na kufuzu kushiriki fainali za Afrika Mashariki mwaka huu.

Fainali za kitaifa zitafanyika wikendi ijayo mjini Kisumu zitakazokutanisha mabingwa wa Mikoa yote nane nchini. Karugwa Girls pia inajivunia kubanduliwa katika fainali za Mkoa wa Mashariki mara mbili kwenye mechi za Chapa Dimba na Safaricom Season One pia Season Two.

Karugwa Girls itashiriki fainali za kitaifa baada ya kuibuka bingwa wa Mkoa wa Mashariki kwenye fainali zilizochezewa Makueni Girls Kaunti ya Makueni. Karugwa Girls ya kocha, Ben Nyongesa akisaidiana na Samson Nyang’aya ilitwaa ubingwa huo ilipobugiza St Mary’s Ndovea kwa bao 1-0 katika fainali.

Ilifuzu fainali ilipolaza Moi Girls Marsabit mabao 2-0 nayo St Marys Ndovea iliirarua Matetei Girls katika nusu fainali ya pili.

”Nilianza kunoa timu hii mwaka jana ambapo kwa mara ya kwanza imepiga hatua katika mashindano ya shule za upili,” kocha huyo alisema na kudai tangu mwaka 2013 imekuwa ikibanduliwa katika Wilaya.

Kuanzia mechi za mashinani hadi kutinga fainali za kitaifa timu hii imetinga magoli 75 na kulazwa mabao matatu.

”Nashukuru wachezaji wangu kwa kazi njema waliofanya mwaka huu kuanzia. Baada ya kufuzu kwa fainali za kitaifa hatuna la ziada mbali tunataka tiketi ya kushiriki ngarambe ya Afrika Mashariki itakayopigiwa nchini Tanzania,” alisema.

Kadhalika alitoa shukrani za dhati kwa wote waliowaunga mkono akiwamo patroni Muthamia Karia, aliyekuwa mwalimu mkuu katika shule hiyo Racheal Riungu, mwalimu mkuu mpya Mary Kaimenyi, wafanyi kazi, bila kusahau Karugwa na Jamii ya Githongo. Anadai kuwa hatua hiyo iliwawapa motisha wa kufanya vizuri.

”Bila kuwasifia wachezaji wetu chini ya nahodha, Verine Achieng wameonyesha wamepania makuu muhula huu pia wamejaa imani watafanya kweli,” Samson Nyang’aya alisema.

Aliongeza hawana hofu yoyote dhidi ya wapinzani wao mbali wanajiandaa kukabili upinzani wowote katika fainali hizo.

Katika fainali za kitaifa, Karugwa Girls imepangwa Kundi A linalojumuisha Nyakach Girls (Nyanza one), Dagoretti Mixed (Nairobi) na Itigo Girls (Mkoa wa Bonde la Ufa).

Kundi B: Kwale Girls (Pwani), Gezero Girls (Nyanza Two), Bishop Njenga Girls (Magharibi) pia bingwa wa Mkoa wa kati.

Karugwa Girls inajumuisha:Jackline Adongo, Christine Oneya, Augusta Nkatha, Sheila Chepchirchir, Winfred Patrick, Lenah Kendi, Brenda Imana, Naomi Njeri, Caroline Kanyeri, Melan Moraa, Pamela Nkirote na Veronica Apondi. Pia wapo Brenda Atieno, Verine Achieng (nahodha), Susan Atero, Cynthia Adhiambo, Lilian Kwamboka, Hope Faith, Brenda Ntinyari na Susan Wanja.

You can share this post!

Fearless yasema ubingwa wa KYSD ni wao msimu huu

GASPO Women wajiahidi kumaliza ndani ya tatu bora

adminleo