Emerging Stars waelekea Uzbekistan kwa mechi za kirafiki
Na GEOFFREY ANENE
TIMU ya taifa ya soka ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 almaarufu Emerging Stars, imefunga safari Jumanne kuelekea nchini Uzbekistan kwa mechi mbili za kirafiki.
Makocha Francis Kimanzi na John Kamau wameamua kutumia wachezaji wengi kutoka Ligi Kuu ya Kenya katika mechi hizo zitakazosakatwa Machi 22 na Machi 25 jijini Tashkent.
Kimanzi hajachuja mchezaji yeyote aliyejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 22 alichotaja Machi 9 kwa michuano hii dhidi ya mabingwa wa Bara Asia, Uzbekistan.
Kenya itapimana nguvu na Uzbekistan kujiweka tayari kwa mechi za kufuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki mwaka 2020 jijini Tokyo nchini Japan.
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) bado halijatangaza ratiba ya mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Afrika la Under-23 litakalotumika kuchagua wawilikishi watatu wa Afrika jijini Tokyo mwaka 2020.
Wanamedali wote watatu katika Kombe la Afrika la Under-23 mwaka 2019 nchini Misri watashiriki makala yajayo ya Olimpiki.
Kikosi cha Kenya:
Makipa
Timothy Odhiambo (Ulinzi Stars), Job Ochieng (Mathare United)
Mabeki
Mike Kibwage (AFC Leopards), Joseph Okumu (hana klabu), Benard Ochieng (Vihiga United), Bolton Omwenga (Kariobangi Sharks), David Owino (Mathare United)
Viungo
Teddy Osok (Sofapaka), Sven Yidah (Kariobangi Sharks), Siraj Mohammed (Bandari), Chrispinus Onyango (KCB), Abdalla Ahmed (Mathare United), Ibrahim Shambi (Ulinzi Stars), James Mazembe (Kariobangi Sharks), Henry Juma (Kariobangi Sharks), Cliff Kasuti (Ulinzi Stars)
Washambuliaji
Pistone Mutamba (Wazito), Amai Atariza (Bandari), Jafari Owiti (AFC Leopards), Brian Yator (KCB), Nicholas Kipkirui (Zoo Kericho), Daniel Okoth Otieno (Sony Sugar).