Michezo

Kocha alalama kutohusishwa na usajili Spurs

August 1st, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

KOCHA Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur ameilaumu klabu hiyo kwa kumpuuza wakati wa shughuli za usajili.

Pochettino alisema hayo baada ya kushuhudia vijana wake wakiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mechi za Audi Cup. Nahodha, Harry alifunga bao hilo.

Spurs waliivunja rekodi yao ya uhamisho kwa kumsajili Tanguy Ndombele kutoka Lyon aliyekubali mkataba wa Sh8.2 bilioni mwezi uliopita, lakini Pochettino amesema hakuhusishwa kwenye shughuli hiyo.

Kocha huyo, alihepa maswali alipoulizwa kuhusu hali ya baadaye ya beki wa pembeni Danny Rose.

“Sina uwezo na kamwe sielewi chochote kuhusu wachezaji wangu wa msimu ujao. Jukumu langu kwa sasa ni kuwanoa tu kwa lengo la kuwaweka katika hali nzuri tayari kwa msimu mpya. Kuhusu uuzaji, usajili na mikataba ya wachezaji sihuzishwi kamwe kwa sasa mamlaka hayo sina, ulizeni mwenyeji wa klabu Daniel Levy maswali hayo.”

Iwapo hali hii itaendelea, itabidi wabadilishe kazi yangu ili nisiendelee kuitwa kocha. Ni kweli mie ndiye bosi anayefaa kuamua wachezaji tutakaokuwa nao, lakini kwa hakika sina uwezo huo kwa sasa.

Mbinu za usajili

Pochettino ambaye awali amewahi kulalamika kutokana na mbinu za usajili kwenye klabu hiyo, alishuhudia vijana wake waliilaza Real Madrid ya kocha Zinedine Zidane 1-0.

Kane alifunga bao hilo muhimu baada ya kukutana na pasi ya Marcelo dakika ya 22 alipoachilia kombora ambalo lilimshinda kipa Keylor Navas.

Katika mechi hiyo, bao la mshambuliaji Rodrygo lilikatiliwa kwa madai kwamba kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alifunga akiwa ameotea.

Kadhalika, Troy Parrott alikosa nafasi ya kufunga bao mechi hiyo ikielekea kumalizika baada ya kombora lake kupiga mlingoti wa goli na kutoka nje.

Rose na Christian Eriksen walianza katika kikosi cha Spurs licha ya uvumi kwamba wanakaribia kuondoka na kujiunga na klabu zingine.

Kwa upande mwingine Madrid walicheza bila Gareth Bale huku Zinedine Zidane akisisitiza kwamba staa huyo alikuwa mgonjwa.

“Bale anaumwa na madaktari walitusihi tumwache apumziko,” alisema kocha huyo. “Alibaki nyumbani kuendelea na mazoezi mepesi. Tulikubaliana hivyo na madaktari wanaomshughulikia baada ya kuzungumza naye binafsi, hivyo ndivyo hali ilivyol.”