Makala

MAPISHI: Kuandaa dagaa kwa kutia sosi ya curry

August 2nd, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • Dagaa kilo 1
  • Pilipili mboga 2
  • Curry powder vijiko 2
  • Limau 1
  • Chumvi
  • Pilipili za kijani; kata vipande vidogovidogo
  • Kitunguu saumu punje 3; menya na saga
  • Nyanya 3 au unaweza kutumia ya kopo
  • Mafuta ya kupikia

Maelekezo

Andaa dagaa kwa kutoa uchafu. Unaweza kukata vichwa kama ukipenda. Osha.

Andaa kitunguu maji kwa kumenya kisha kata vipande vidogo. Kata pilipili mboga vipande vidogo.

Bandika kikaangio mekoni, weka mafuta kiasi kisha weka kitunguu saumu halafu ukoroge. Weka kitunguu maji kisha acha viive kwa dakika tatu.

Ongeza chumvi kisha weka dagaa kwenye sufuria. Koroga vizuri kisha funika na acha dagaa wakaangike kiasi kwenye mafuta.

Ongeza nyanya, koroga pamoja vichanganyike kisha funika acha ziive. Hakikisha hazikauki ,unaweza kuongeza maji kiasi ili ziendelee kuiva vizuri.

Baada ya dakika kama 10 ongeza pilipili mboga, karoti na pilipili ndefu za kijani. Koroga vizuri kisha funika.

Sosi ya nyanya ikishaiva, weka curry powder. Koroga pamoja kisha kamulia limau. Unaweza kuweka nusu ili mboga isiwe chachu sana. Koroga vizuri.

Acha ichemke kwa dakika 10.

Pakua na ugali na ufurahie.