• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Chapa Dimba Season Three kuanza Septemba

Chapa Dimba Season Three kuanza Septemba

Na JOHN KIMWERE

KAMPUNI ya simu za rununu ya Safaricom, imetangaza kwamba itaendelea kushirikiana na Ligi ya LaLiga ya Hispania na Shirikisho la Soka ya Kenya (FKF) kuandaa kinyang’anyiro cha Chapa Dimba na Safaricom Season Three. Mashindano hayo hushirikisha timu za wavulana na wasichana kwa wasiozidi umri wa miaka 20 kote nchini.

Michuano hiyo huanzia mashinani katika mikoa nane nchini huku timu ambazo huibuka mabingwa zikifuzu kushiriki fainali za kitaifa kuwakilisha mikoa yao.

Kadhalika Safaricom imetangaza kwamba msimu huu itaandaa mafunzo kwa makocha wa timu zote zitakazoshiriki ngarambe hiyo. ‘

Joy Queenlady (kulia) wa Chama Dimba Allstars akishindana na Beverly Rowa wa Safaricom Allstars ya kuzindua kipute cha Chapa Dimba na Safaricom Season Three katika Uwanja wa Ligi Ndogo, Nairobi. Picha/ John Kimwere

‘Chapa Dimba ni mradi wa kukuza talanta za wachezaji chipukizi mashinani ambapo tunashukuru Safaricom kwa kujitolea kuandaa na kudhamini makala mengine. Bila shaka tutaendelea kuunga mkono hatua ya kukuza vipaji vya wachezaji wazuri mashinani,” rais wa FKF, Nick Mwendwa alisema kwenye uzinduzi wa kipute cha muhula huu 2019/2020.

Naye ofisa mkuu wa Safaricom kitengo cha wateja, Sylvia Mulinge alisema “Chapa Dimba inatoa matumaini ya maisha mazuri kwa vijana wengi nchini maana tumegundua umuhimu wa spoti ambapo tunaamini kwamba inasadia wengi kupata ajira na kujikimu kimaisha.”

Mechi za viwango vya mashinani zitaanza mapema mwezi ujao nazo fainali za kitaifa zimeratibiwa kuandaliwa tarehe sita na saba Juni 2020 mjini Mombasa. Zaidi ya timu 3000 zinatazamiwa kujiandikisha kushiriki mashindano ya msimu huu.

You can share this post!

Pro Soccer yalenga kubeba taji la KYSD

Kenya yafundishwa magongo

adminleo