Makala

ULIMBWENDE: Jinsi ya kujifanyia ‘facial’ nyumbani

September 10th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

BAADHI ya watu wana mazoea ya kwenda saluni kufanyiwa mambo kadha wa kadha yanayohusu urembo kama vile kuosha na kusuka nywele, kwenda kufanyiwa masaji pamoja na matibabu ya ngozi hasa usoni.

Bila shaka pesa zinahitajika kufanikisha hayo yote. Hata hivyo, iwapo huna pesa, unaweza kujifanyia vyote mwenyewe nyumbani tena kwa kutumia vitu ambavyo unavyo tayari.

Huu hapa utaratibu wa jinsi ambavyo unafaa kufanya:

Ondoa vipodozi na usafishe uso

Kabla ya kufanya lolote, kwanza kama ulikuwa na vipodozi usoni inabidi uviondoe ili kuwezesha mzunguko mzuri wa hewa.

Namna ya kutumia mafuta ya nazi kuondoa vipodozi:

  • Chukua pamba uitumbukize katika mafuta ya nazi
  • Anze kufuta uso wako taratibu

Safisha uso.

Ili kujiandaa kwa ajili ya ‘facial’ ni lazima usafishe uso wako vizuri kwa sabuni ili kuondoa mafuta ya nazi au make up remover.

Unaweza pia kutumia asali.

Namna ya kutumia asali kusafisha uso

  • hakikisha umesha osha uso wako vizuri
  • chukua kijiko kimoja cha asali na uanze kupaka usoni
  • sugua taratibu kwa dakika tano ili kuondoa ngozi zilizo kufa lakini pia kuzibua vinyweleo vya ngozi vilivyo zibika

Mvuke

Chukua nguo safi au taulo uweke katika maji ya vuguvugu halafu kausha kidogo na uweke usoni.

Pia unaweza kuchemsha maji ukayamimina kwenye beseni au bakuli kubwa na kuliinamia ili upate mvuke.

Fanya hivi kwa muda wa robo saa.

Maski

Kwa wenye ngozi za mafuta, wanaweza kujaribu clay mask ili kunyonya au kufyonza mafuta katika ngozi zao.

Kwa ngozi kavu itabidi utumie maski ambazo zinasaidia kuongeza maji na mafuta katika ngozi yako.

Paka maski yako kwa takriban robo saa na uoshe uso wako na kuukausha.

Paka mafuta

Hatua hii ni muhimu ili kuilanisha ngozi yako na kuifanya ipendeze.