Michezo

Rudisha nje Kenya ikichagua kikosi cha Riadha za Dunia 2019

September 13th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na GEOFFREY ANENE

KENYA ni nchi ya hivi punde baada ya mahasimu wa tangu jadi Ethiopia, Australia na Jamaica kuchagua timu itakayoiwakilisha kwenye Riadha za Dunia zitakazofanyika jijini Doha nchini Qatar mnamo Septemba 27 hadi Oktoba 6, 2019.

Mabingwa wa dunia mwaka 2015 Kenya watawakilishwa katika mbio za mita 400 hadi kilomita 42 (marathon) katika makala hayo ya 17.

Washindi wa michezo ya Afrika (African Games) George Manangoi (mita 1,500), Benjamin Kigen (mita 3,000 kuruka viunzi na maji), Samuel Gathimba (matembezi ya kilomita 20), Julius Yego (urushaji wa mkuki) na Lilian Kasait (mita 5,000) wamo kikosini, ingawa Emily Ngii (matembezi ya kilomita 20) na Vanice Kerubo (mita 400 kuruka viunzi) wako nje.

Mfalme mara mbili wa mbio za mita 800 wa Afrika, Dunia na Olimpiki, David Rudisha, pia hakufuzu.

Kikosi cha Kenya:

Wanariadha

Mita 400 – Alphas Kishoyian, Emmanuel Korir (wanaume), Hellen Syombua, Mary Moraa (wanawake);

Mita 800 – Ng’eno Kipng’etich, Emmanuel Korir, Ferguson Rotich (wanaume), Eunice Sum, Jackline Wambui (wanawake);

Mita 1,500 – Elijah Manangoi, Timothy Cheruiyot, Ronald Kwemoi, George Manangoi (wanaume), Faith Chepng’etich, Winnie Chebet (wanawake);

Mita 3,000 kuruka viunzi na maji – Conseslus Kipruto, Leonard Bett, Benjamin Kigen, Abraham Kibiwott (wanaume), Beatrice Chepkoech, Hyvin Kiyeng, Celliphine Chespol, Fancy Cherono (wanawake);

Mita 5,000 – Nicholas Kipkorir Kimeli (wanaume), Hellen Obiri, Lilian Kasait, Margaret Chelimo (wanawake);

Mita 10,000 – Rhonex Kipruto, Rodgers Kwemoi, Alex Oloitiptip (wanaume), Agnes Jebet Tirop, Hellen Obiri, Rosemary Wanjiru (wanawake);

Matembezi ya kilomita 20 – Samuel Gathimba (mwanamume), Grace Wanjiru (mwanamke);

Marathon – Geoffrey Kirui, Amos Kipruto, Paul Lonyangata, Laban Korir (wanaume), Ruth Chepng’etich, Edna Kiplagat, Visiline Jepkesho (wanawake);

Mbio za wanaume kwa wanawake za kupokezana vijiti – Alphas Kishoyian, Alex Sampao, Joseph Poghisio, Mary Moraa, Gladys Musyoki;

Kurusha mkuki – Julius Yego (mwanamume);

Kuruka Juu (High Jump) – Matthew Sawe (mwanamume);

Maafisa – Julius Kirwa (kocha mkuu), Richard Metto, Joseph Cheromei, Abraham Kiplimo, Ben Ouma, Shem Kororia, David Kitur, Sheila Kalunda, William Tanui, Silas Kiambata, Gedion Nyangech (makocha wasaidizi), – Joseph Kiget (meneja wa timu), Erastus Kabugi (meneja wa timu msaidizi), Peninah Talam, (Chaperone) Fred Oudo, Nahashon Kibon (maafisa wa kutoa stakabadhi)