• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 2:07 PM
Harambee Starlets kukabiliana na Black Queens ya Ghana mnamo Oktoba 4 na 8

Harambee Starlets kukabiliana na Black Queens ya Ghana mnamo Oktoba 4 na 8

Na GEOFFREY ANENE

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza tarehe za mechi za kufuzu kushriki michezo ya Olimpiki mwaka 2020 kati ya Harambee Starlets ya Kenya na Black Queens ya Ghana.

Raundi hiyo ya tatu itafanyika Oktoba 4 (mechi ya mkondo wa kwanza) nchini Ghana na Oktoba 8 (mechi ya marudiano) nchini Kenya.

Starlets, ambayo ilibandua nje She-Flames ya Malawi katika raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 5-3, itaelekea nchini Ghana mnamo Oktoba 2 na kurejea Oktoba 5.

Vipusa wa kocha David Ouma walikaba Ghana 1-1 mara ya mwisho walikutana katika mechi ya kirafiki uwanjani Kasarani katika ya Kombe la Afrika (AWCON) mwaka 2018 kuanza.

Starlets ilichapa Ethiopia 3-2 katika mechi ya kujipima nguvu kabla ya kuvaana na Malawi. Ilipoteza dhidi ya She-Flames katika mechi ya mkondo wa kwanza 3-1 jijini Blantyre kabla ya kulipiza kisasi kwa kuifunga 3-0 katika mechi ya marudiano uwanjani Kenyatta mjini Machakos.

Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) halijatangaza iwapo Starlets itapata mechi ya kujipima nguvu kabla ya kuelekea Ghana, ambayo ilipepeta Togo 4-1 katika mechi ya kirafiki mnamo Septemba 14. Wachezaji Evelyn Badu na Gladys Amfobea walifunga mabao mawili kila mmoja dhidi ya Togo iliyojiliwaza na bao kutoka kwa Adina Akakpo.

Mshindi kati ya Kenya na Ghana ataingia raundi ya tatu na akifanya vyema atashiriki raundi ya nne halafu ya tano, ambayo atakayeibuka mshindi atajikatia tiketi ya kuwa jijini Tokyo nchini Japan kwa Olimpiki.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge waliodaiwa kuchochea chuki waachiliwa

Kivumbi chatarajiwa Thika Queens na Gaspo Women wakivaana

adminleo