• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 1:13 PM
Joe na Edward watetemesha Super 8

Joe na Edward watetemesha Super 8

Na JOHN KIMWERE

WANASOKA Joe Abong’o na Edward Peter kila mmoja alipiga kombora moja safi kwenye mechi za Super Eight Premier League (S8PL) na kubeba Githurai Allstars na Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Kenya (TUK) kuzoa alama tatu muhimu.

Githurai Allstars na TUK kila moja ilijiongezea ufanisi huo baada ya kufunika kimiani bao 1-0 dhidi ya Lebanon FC na Mathare Flames mtawalia.

Nao mabingwa watetezi, Jericho Allstars ambayo hunolewa na kocha, Thomas Okongo ilionyesha kivumbi kikali na kukubali kulala kwa magoli 2-0 mbele ya majirani zao Madakara J.L.S.A kwenye patashika iliyopigiwa Camp Toyoyo Jericho, Nairobi.

Mchezaji wa NYSA (kulia) ashindana na mpizani wake wa Githurai Allstars kwenye mechi ya kuwania taji la S8PL. Picha/ John Kimwere

”Kusema kweli nawapawa hongera wachezaji wangu wanaendelea kukazana kwa udi na uvumba kukabili wapinzani wetu kwenye mechi za muhula huu,” alisema kocha wa Githurai Allstars, Geoffrey Onyango na kuongeza kuwa wamepania kuendeleza mtindo huo ili kutimiza azimio lao.

Kwa upande wa TUK, kocha wake, Luke Aluoch alisema “Ingawa tumejikuta pambaya mbele ya wapinzani wetu nashukuru kikosi changu kwa jumla kinaendelea kuonyesha dalili za kuzinduka.”

Wachana nyavu wa Makadara J.L.S.A wanaoketi katika mduara hatari wa kuteremshwa daraja walifanya kweli kuangusha wanzao hao kupitia juhudi Kaycy Odhiambo na Erickson Kamweru walipocheka na nyavu mara moja kila mmoja.

Kwenye mfululizo wa matokeo hayo, NYSA ya kocha, Fredrick ‘Oti’ Otieno iliangukia pua iliponyukwa mabao 2-0 na MASA, nacho kikosi cha Meltah Kabiria kinaokuja kwa kasi msimu huu kilichomokla na ushindi wa magoli 3-2 mbele ya Huruma Kona.

Mchezaji wa Kawangware United (kulia) akishindana na mwenzake wa Meltah Kabiria kwenye mechi ya S8PL. Jumapili iliyopita Meltah Kabiria ilishinda Huruma Kona mabao 3-2. Picha/ John Kimwere

Nayo Rongai Allstars ilishindwa kufana na kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 Shauri Sportiff.

MATOKEO YA WIKENDI

Mathare Flames 0-1 TUK

Madakara J.L.S.A 2-0 Jericho Allstars

MASA 2-0 NYSA

Meltah Kabiria 3-2 Huruma Kona

Githurai Allstars 1-0 Lebanon FC

Rongai Allstars 1-1 Shaurimoyo Sportif FC

You can share this post!

Ngarambe ya Super 8 yaanza

Uganda, Burundi wavuna ushindi Cecafa U20 ikipamba moto

adminleo