• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Kimanzi ataja vifaa 23 vya kukabili Msumbiji kirafiki

Kimanzi ataja vifaa 23 vya kukabili Msumbiji kirafiki

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA Francis Kimanzi amefanyia kikosi chake cha Harambee Stars mabadiliko makubwa katika idara ya ulinzi akitaja timu ya wachezaji 23 itakayopimana nguvu na Msumbiji kujiandalia mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (Afcon) mwaka 2021.

Kipa Patrick Matasi, ambaye kwa muda mrefu amekuwa nambari moja, ameachwa nje, huku tetesi zikidai yuko mbioni kuagana na miamba wa Ethiopia, Saint George.

Matasi pamoja na John Oyemba (Kariobangi Sharks) na Farouk Shikalo (Young Africans, Tanzania) walikuwa katika Afcon nchini Misri mwezi Juni-Julai.

Katika idara hiyo, Shikalo pekee ndiye amebaki kikosini. Hata hivyo, Kimanzi amemwita mmoja wa makipa waliozungumziwa sana, akitakiwa kutajwa, Ian Otieno. Kipa huyu wa Red Arrows nchini Zambia amekuwa nje kwa muda mrefu.

Mbali na Otieno, Timothy Odhiambo wa Ulinzi Stars pia atapigania nafasi ya kuwa michumani dhidi ya Msumbiji mnamo Oktoba 13.

Odhiambo alikuwa katika timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 almaarufu Emerging Stars, lakini ni mara yake ya kwanza katika Harambee Stars.

Wachezaji wengine, ambao wamerejea kikosini ni beki Harun Shakava anayechezea Nkana nchini Zambia, mshambuliaji Masoud Juma wa JS Kabylie nchini Algeria na beki Yusuf Mainge, ambaye ni mali ya FK Pohronie nchini Slovakia).

Kiungo Ayub Timbe atakosa mechi hiyo. Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limesema kuwa klabu yake ya Beijing Renhe, ambayo inakabiliwa na hatari ya kutemwa kutoka Ligi Kuu ya Uchina imeomba asihusishwe inapojiandaa kuvaana na Chongqing Lifan hapo Oktoba 13.

Kiungo wa Tottenham Hotspur, Victor Wanyama pia ameitwa. Stars itaingia kambini Oktoba 7 kabla ya kualika Msumbiji uwanjani Kasarani Oktoba 13.

Kenya iko Kundi G pamoja na Misri, Togo na Comoros katika mechi za kufuzu.

Kikosi

Makipa – Ian Otieno (Red Arrows, Zambia), Timothy Odhiambo (Ulinzi), Faruk Shikalo (Yanga, Tanzania);

Mabeki – Johnstone Omurwa (Wazito), Harun Shakava (Nkana, Zambia), Joash Onyango (Gor), Yusuf Mainge (FK Pohronie, Slovakia), Hillary Wandera (Tusker), Erick Ouma (Vasalunds IF, Uswidi), Joseph Okumu (IF Elfsborg, Uswidi), Samuel Olwande (Kariobang);

Viungo – Anthony Akumu (Zesco, Zambia), Abdallah Hassan (Bandari), Kenneth Muguna (Gor), Duke Abuya (Kariobangi), Victor Wanyama (Tottenham Hotspur), Clifton Miheso (Gor), Lawrence Juma (Gor), Cliff Nyakeya (FC Masr, Misri), Whyvone Isuza (AFC Leopards);

Washambuliaji – Michael Olunga (Kashiwa Reysol, Japan), Jesse Were (Zesco), Masoud Juma (JS Kabylie, Algeria).

You can share this post!

Starlets wana matumaini kwamba mara hii watazima Waghana

Macho yote kwa Conseslus mbio za mita 3000 kuruka viunzi

adminleo