SIHA NA ULIMBWENDE: Manufaa ya mafuta ya mbegu za alizeti (sunflower)
Na MARGARET MAINA
KWA kutunza ngozi yako, mafuta ya mbegu za alizeti ni chanzo muhimu cha vitamini E, yenye virutubisho na antioxidants, na inafaa katika kupambana na chunusi, uvimbe, wekundu kwa jumla na kuwasha kwa ngozi.
Husaidia kuweka unyevu kwenye ngozi yako
Mafuta ya alizeti yana ubora wake wa kusaidia ngozi kuhifadhi unyevu wake. Vitamini E husaidia kuvuta unyevu ndani ya seli za ngozi, na kutunza unyevu wa ngozi kwa muda mrefu.
Yana wingi wa vitamini E
Wingi wa vitamini E antioxidant katika alizeti husaidia kulinda seli za ngozi kutokana na mionzi hatari ya jua ‘UV rays’ na mengine hatari kutoka kwenye mazingira.
Husaidia kupambana na chunusi
Mbali na vitamini E, mafuta ya alizeti pia yana vitamini A, C, na D, na hivyo ni bora katika matibabu ya chunusi.
Mafuta ya mbegu za alizeti yana vitamini na asidi ya mafuta ambayo hufanya kama antioxidants kutengeneza seli mpya za ngozi na kusaidia ngozi yako kuondoa bakteria wanaosababisha chunusi.
Yanaweza kupunguza dalili za kuzeeka na makunyanzi
Sifa ya antioxidant ya mafuta ya alizeti ni kwamba husaidia katika kuzuia ishara za kuzeeka mapema. Hii ni kwa sababu husaidia kulinda ngozi kutokana na udhihirisho wa jua.
Vitamini E katika mafuta ya mbegu za alizeti inaweza kusaidia kulinda collagen na elastin kwenye ngozi na kupunguza muonekano wa mistari au makunyanzi na kasoro zinginezo kwenye uso wa mtumiaji.
Mafuta ya mbegu ya alizeti ni muhimu kwa ngozi kavu.
Mafuta ya alizeti yana ‘maliasili’ ya kutuliza ambayo inaboresha uwezo wa kuhifadhi unyevu wa ngozi yako na inafaa kwa watu walio na ngozi isiyo na maji au nyeti.
Kutumia mafuta ya alizeti mara kwa mara kunaweza kusaidia kuondoa seli zilizokufa na uchafu, na kuacha ngozi laini na yenye unyevu.
Husaidia kutuliza na kuponya ngozi yako
Mafuta ya mbegu ya alizeti yana wingi wa asidi ya mafuta ya omega-6 (linoleic) na asidi ya vitamini omega-6 husaidia kupungua kwa kuvimba kwenye ngozi na inakuza ukuzaji wa seli mpya za ngozi.
TAHADHARI: Matumizi ya mafuta haya kupita kiasi kwenye ngozi yako yanaweza KUkuziba tundu za uso wako na kukuongezea chunusi. Tumia kwa uangalifu.