Morans yafufua uhasama dhidi ya Uganda
Na GEOFFREY ANENE
MORANS ya Kenya inafufua uhasama dhidi ya Uganda katika mechi ya ufunguzi ya raga ya kimataifa ya wachezaji saba kila upande ya Safari Sevens uwanjani RFUEA jijini Nairobi, Jumamosi.
Timu ya Morans italenga kuwa na mwanzo mzuri hasa kwa sababu Uganda na Burundi ndizo timu zinazoonekana rahisi ikilinganishwa na miamba Afrika Kusini ambao ni tisho kubwa sio tu katika Kundi A, bali katika mashindano haya.
Morans na Uganda zinafahamiana kutoka mechi za makundi za mwaka 2018 ambapo Morans iliponyoka na ushindi wa alama 19-12 katika mechi ngumu.
Licha ya kuwa timu ya pili ya Kenya, Morans inajivunia wachezaji matata kama Jeff Oluoch, Vincent Onyala, Johnstone Olindi na Geoffrey Okwach.
Timu ya kwanza ya Kenya almaarufu Shujaa itavaana na Zambia, ambao wanarejea katika mashindano haya baada ya kuwa nje muda mrefu, timu ya Russia Academy inayoongozwa na shujaa wa Fiji, Waisale Serevi, na Blue Bulls kutoka Afrika Kusini. Shujaa inajumuisha wachezaji wengi walio na uzoefu kama Andrew Amonde, Collins Injera, William Ambaka, Jacob Ojee na Nelson Oyoo. Leo Oktoba 18 Injera, ambaye wakati mmoja alikuwa mfungaji wa miguso mingi kwenye Raga ya Dunia, alisherehekea kufikisha miaka 33 tangu azawaliwe.
Uganda inanolewa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Tolbert Onyango. Mabingwa wa raga ya wachezaji saba kila upande wa Ufaransa, Seventise, pia wako chini ya mchezaji wa zamani wa Kenya, Teddy Omondi.
Timu za Morans na Shujaa ziko chini ya raia wa New Zealand, Paul Feeney.
Ratiba (kuanzia saa tatu na nusu asubuhi):
Uganda na Morans (Kenya)
Afrika Kusini na Burundi
Western Province (Afrika Kusini) na Zastava (Urusi)
Samurai (Uingereza) na Red Wailers (Uingereza)
Blue Bulls (Afrika Kusini) na Russia Academy (Urusi)
Shujaa (Kenya) na Zambia
Zimbabwe na Seventise (Ufaransa)
Uhispania na KCB (Kenya)
Uganda na Burundi
Afrika Kusini na Morans
Western Province na Red Wailers
Samurai na Zastava
Blue Bulls na Zambia
Shujaa na Russia Academy
Zimbabwe na KCB
Uhispania na Seventise
Morans na Burundi
Zastava na Red Wailers
Russia Academy na Zambia
Seventise na KCB
Afrika Kusini na Uganda
Samurai na Western Province
Shujaa na Blue Bulls
Uhispania na Zimbabwe
VIKOSI VYA KENYA:
Shujaa – Andrew Amonde (nahodha), Bush Mwale , William Ambaka, Brian Wandera, Charles Omondi, Collins Injera, Mickey Wanjala, Daniel Taabu,Oscar Denis, Nelson Oyoo, Mike Okello, Jacob Ojee.
Morans – Jeff Oluoch (nahodha), Vincent Onyala, Alvin Otieno, Timothy Mmasi, Dan Sikuta, Monate Akwei, Herman Humwa, Ian Mabwa, Davis Nyaundi, Johnstone Olindi, Geoffrey Okwach, Joel Inzuga, Collins Shikoli.