• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
CITY NOMA: Manchester City yaipiga Atalanta 5-1

CITY NOMA: Manchester City yaipiga Atalanta 5-1

Na MASHIRIKA

MANCHESTER, Uingereza

STRAIKA Raheem Sterling alifunga mabao matatu kwa mara ya kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya na kuisaidia klabu yake ya Manchester City kuibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya Atalanta ya Italia katika pambano la Kundi C.

Sergio Aguero aliongeza mabao mawili.

Atalanta ilifunga penalti kupitia kwa Ruslan Malinovskyi baada ya Fernandinho kumuangusha Josip Ilicic. Sterling ambaye ndiye mfungaji wa mabao mengi ya City baada ya kuifungia klabu hiyo ya EPL mara 12 katika mechi 13 za mashindano tofauti, msimu huu alisema kuna mengine mazuri njiani.

Kocha wake, Pep Guardiola alimsifu kama mchezaji aliyeimarika zaidi kutokana na nguvu zake za ziada awapo uwanjani.

Kwenye mechi hiyo, Rodri aliondolewa baada ya kuumia, huku Phil Foden akionyeshwa kadi nyekundu, hii ikiwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka.

“Ana nguvu za kucheza hata mechi mbili mfululizo, mwenye mbio za kutisha. Ni mchezaji wa kipekee.” Guardiola alianza na Fernandinho kama beki wa katikati, huku Kyle Walker na Benjamin Mendy wakicheza kama mabeki wa pembeni.

Timu hizi zitakutana tena hapo Novemba 6 nchini Italia katika mechi ambayo City watatinga hatua ya 16 Bora iwapo wataibuka na ushindi.

Kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Foden, kocha huyo alisema hatamuadhibu kutokana na kosa alilofanya, lakini atamshauri awe makini zaidi akiwa na kadi ya njano.

“Siwezi kumuadhibu kwa sababu alicheza vizuri zaidi na kufanya safu ya kiungo kuvuma kabla ya kutolewa. Sio rahisi mimi kumuadhibu mchezaji, pengine kama amefanya kosa ya kiujinga.”

“Kuna wale wanaofikiria ni lazima apewe muda mrefu wa kucheza, lakini lazima wajiulize maswali kama kiwango chake kiko vipi akilinganishwa na David Silva, Ilkay Gundogan au Kevin de Bruyne.

“Angali na muda wa kutosha kujifunza zaidi. Lazima aelewe anapokuwa na kadi ya njano, ni vyema kucheza kwa tahadhari, hasa ikikumbukwa kwamba tulikuwa tukiongoza kwa 5-1, lakini mambo yanapokuwa 2-1 au 3-2, hali inakuwa ngumu.”

Kocha huyo alisema sasa mawazo yao yanaelekea kwa ligi kuu ya Uingereza wanakoshikilia nafasi ya pili nyuma ya Liverpool kwa tofauti ya pointi tatu. City wamepangiwa kukutana na Aston Villa, Jumamosi.

 

Matokeo kwa ufupi yalikuwa:

Atletico 1 Leverkusen 0; Shakhtar 2 Dinamo Zagreb 2; Club Brugge 0 PSG 5; Galatasaray 0 Real Madrid 1; Juventus 2 Lokomativo Moscow 1; Manchester City 5 Atalanta 1; Olympiakos 2 Bayern 3; Spurs 5 Read Stars Belgrade 0.

You can share this post!

KIU YA UFANISI: Aliona washonaji nguo ni wengi, akaamua...

Koplo Caroline Mango Atieno aachiliwa kwa dhamana ya Sh2...

adminleo