• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
AKILIMALI: Mitambo hii ndiyo jibu la matatizo yako ya kilimo

AKILIMALI: Mitambo hii ndiyo jibu la matatizo yako ya kilimo

Na BRIAN OKINDA na CHARLES WASONGA

WAKATI wa mafunzo ya kilimo nyanjani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Egerton, Kaunti ya Nakuru hivi majuzi, palitokea nafasi kwa wakulima kujionea mitambo ya kiteknolojia ambayo wakiitumia wataweza kujitosholeza kwa chakula na taifa kwa jumla.

Mafunzo hayo ambayo maudhui yake yalikuwa ni uimarishaji wa uzalishaji wa chakula kupitia teknolojia na ubunifu, yalihusu mbinu za kisasa ambazo zitawakinga wakulima na wafugaji kupata hasara inayosabishwa na mabadiliko katika hali ya anga.

Baadhi ya mbinu za kilimo walizofunzwa ni kilimo hifadhi (conservation agriculture) ambacho lengo lake ni huhimiza matumizi ya rasilmali chache kwa uangalifu ili kuzalisha faida kubwa bila kuiharibu rasilmali hiyo.

Kulingana na Brian Sakwa, mtaalamu wa kilimo anayehudumu katika Shirika la Utafiti kuhusu Kilimo na Ufagaji (Kalro), kituo cha Njoro, aina hii ya kilimo ina manufaa mengi.

Miongoni mwa manufaa hayo ni; kuimarika kwa uzalishaji, kupungua kwa gharama ya uzalishaji, na kutoharibika haraka kwa mashine inayotumika shambani.

Wakulima wanahimizwa kutumia mashine nyepesi au ndogo kulima mashamba yao kwa sababu, kulingana na Bw Sakwa, mashine nzito zinaweza kusababisha mchanga kuwa mgumu. Hali hii inaweza kuathiri mavuno hasa ya mimea ya shambani.

“Wakulima wa mimea ya vyakula wanashauriwa kutumia mashine nyepesi isiyo na madhara kwa mchanga. Mimea ya vyakula inahitaji mchanga mwororo,” akaeleza.

Baadhi ya mitambo na vifaa ambavyo wakulima walipata fursa ya kujionea wakati wa mafunzo hayo ni kama vile;

Jokofu la kuhifadhi maziwa linalotumia kawi ya jua (Solar milk cooler)

Mtambo huu hutumia kawi ya jua yaani sola. Imeundwa kwa namna ya kipekee hivi kwamba unaweza kuhifadhi maziwa kwa siku tatu bila kutumia mwangaza wa jua.

Hii ni kwa sababu unaweza kuhifadhi kawi ya jua katika kifaa kinachojulikana kama “ice bank” badala ya betri. Unaweza kugeuzi asilimia 20 ya kawi ya sola kutoka paneli na kuwa barafu.

Mkulima (kulia) awasikiliza wataalamu wakielezea jinsi ambavyo mashine huchanganya chakula cha mifugo wakati wa maonyesho katika Chuo Kikuu cha Egerton. Picha/ Brian Okinda

Mtambo huo ulivumbuliwa na Dkt Musa Njue anayehudumu katika idara ya Uhandishi wa Kilimo katika Chuo Kikuu cha Egerton. Kuna aina mbili; wenye uwezo wa kuhifadhi kati ya lita 300 za maziwa na ule ambao unaweza kuhifadhi lita 500 za maziwa.

“Mitambo hii ni bora kwa makundi ya vijana na wanawake na wakulima wa kiwango kidogo. Vyama vya ushirika vya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa pia vinaweza kuutumia. Itawafaa wakulima kwa sababu wataokoa gharama ya stima, jenereta na unaweza kudumu kwa hadi miaka 20,” akasema Dkt Njue.

Mtambo maalum wa kunyinyiza (“Pedestal sprayer”)

Huu ni mtambo ambao kulingana na Bw Sakwa, unarahisisha shughuli za unyunyizaji dawa kwa mimea shambani. Hii ni kwa sababu unaweza kuendeshwa na mtu mmoja na kuweza kunyunyiza sehemu kubwa wakati mmoja.

Umewekwa troli kubwa inayotoshana na baiskeli ndogo. Mtungi (knapsack) wenye uwezo wa kubeba kati ya lita 20 hadi lita 60 ya mchanganyiko wa kemikali umewekwa kwenye troli giyo. Na pampu imeweka karibu na mtungi.

Mkulima anaweza kuendesha mtambo huo huku ukitoa michirizi ya dawa kupitia bomba. Mtambo huo ni rahisi kutumia kwa sababu unaweza kuendeshwa ndani ya mistari ya mimea.

“Ni rahisi kuutumia kwa sababu hauhitaji kawi kwa sababu ni huzunguka kwa magurudumu yake katika harakati ya kupiga kemikali kutoka kwa mtungi na kunyunyizia mimea,” akasema Bw Sakwa.

Mtambo wa kutoa uchafu kutoka kwa nafaka (Grain winnower)

Mtambo huu husaidia sana katika shughuli ya kutoa uchafu kutoka kwa mafaka, hasa mahindi.

Una sehemu kama vile mortar, blower, pulley, dust outlet, inlet hopper na clean grain hopper.

Nafaka humwagwa ndani ya “inlet hopper” na “blowers” zilizotundikwa katika “hopper” na motor huendeshwa ili kutoa vumbi na uchafu ndani ya nafaka.

“Mtambo huu unaweza kutumiwa kusafisha mahindi, wimbi, mbegu za alizeti, mbegu za mchicha (terere), maharagwe miongoni mwa aina nyingi za nafaka haraka na kwa gharama ya chini,” akasema Bw Sakwa.

Mtambo wa kuchanganya lishe ya mifugo (Feed Mixer)

Mtambo huo umeundwa ili kuweza kuchanganya aina mbalimbali ya lishe kama vile lishe ya ng’ombe, nguruwe, kuku na hata chakula cha binadamu, kulingana na Dkt Njue.

“Baadhi ya wakulima wabunifu hata huitumia kuchanganya mchanga na mbolea kwa ajili ya kuandaa miche kwenye mifuko au mikebe,” anaongeza.

Kuna mitambo ambayo inaweza kuandaa kilo 250 ya lishe, kilo 600, na kilo 1,000, kwa muda wa saa moja.

Mtambo wa kupanda unaokokotwa kwa ng’ombe (Animal drawn no-till planter)

Mtambo huu umetengenezwa kwa muundo wa jembe la kawaida la kukokotwa kwa ng’ombe.

Una sehemu maalum ya kuweka mbegu na mbolea na kisahani cha kufunika mbegu baada ya kudondoshwa kwenye mashimo wakati wa upanzi.

Bw Peter Kiprotich, mtaalamu ambaye anahudumu katika kituo cha Kalro, Njoro, anasema mtambo huo unapokokotwa shambani kisahani cha kwanza hutengeneza laini na mashimo, kisha mbegu na mbolea hudondoka ndani ya mashimo hayo kabla ya kisahani cha mwisho kuyafunika mashimo hayo.

“Mtambo huo hupunguza idadi ya wafanyakazi wanaohitajika kwa sababu huendeshwa na watu wawili pekee,” asema Kiprotich huku akiongeza kuwa kwa kutumia kifaa hicho, mkulima hahitaji kulima shamba lake.”

Mitambo mingine ambayo wakulima waliweza kuonyeshwa ni ile ya kuvuna na kutayarisha mtama/pojo//wimbi, nyingi zikiendeshwa kwa nguvu za upepo (kwa Kiingereza huitwa Sorghum/green-gram/finger-millet thresher na Pneumatic chaff-cutter).

Sorghum thresher hutumika kuvuna na kutayarisha mtama na wimbi huku Chaff-Cutter ikitumika kukata nyasi ya kulisha ng’ombe.

You can share this post!

MAKALA MAALUM: Nyandarua yalemewa na visa vya mauaji na...

KILIMO NA BIASHARA MASHINANI: Kilimo cha mboga za aina...

adminleo