• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Bandari, Storms watia fora vikapuni

Bandari, Storms watia fora vikapuni

Na CAXTON APOLLO

TIMU za mpira wa vikapu za Bandari na Storms ziliingia nusu-fainali ya Ligi Kuu ya wanawake baada ya kung’aa katika robo-fainali jijini Nairobi, wikendi.

Bandari walibandua wenyeji wao Eagle Wings 2-0 katika mfululizo wa mechi tatu za robo-fainali.

Ilifunga Wings 78-43 katika mechi ya kwanza Jumamosi.

Bandari, ambayo ilipoteza ubingwa kwa kulazwa 3-1 dhidi ya Equity Bank katika fainali ya mwaka jana, haikulegeza kamba katika mechi ya pili ambapo ililaza Wings 79-31 Jumapili.

Katika mechi ya pili, mlinzi mwepesi Hilda Indasi aliifungia Bandari pointi 26. Bandari iliongoza 38-29 kufikia muda wa mapumziko. Wings, ililemewa na Bandari katika robo ya tatu, 19-0.

Bandari iliwatumia Natalie Akinyi, Indasi na Brenda Angeshi kuwafunga wapinzani wake alama zaidi 22 dhidi ya 12 kwenye robo ya nne. Storms ilijikatia tiketi baada ya kuzaba Chuo Kikuu cha Strathmore kwa mechi 2-1.

Katika mechi ya tatu ya kuamua mshindi, Cylia Atieno alifunga pointi 14 naye Pamela Sinda akaongeza alama 10 na kuiwezesha Storms kulaza Strathmore 66-62.

Storms,iliyokamilisha msimu wa kawaida katika nafasi ya sita, ilianza robo-fainali kwa kushindwa 42-39 na Strathmore.

Storms yaamka mechi ya

Hata hivyo, Storms ya kocha Abel Nson iliamka katika mechi ya pili na kushinda 70-54. Storms ilimaliza katika nafasi ya tatu mwaka jana.

Katika robo-fainali ya ligi kuu ya wanaume, mabingwa watetezi Bandari walianza kampeni ya kuwa timu ya tatu kushinda ubingwa mara nne mfululizo baada ya kulima wenyeji Blades ya Chuo Kikuu cha Strathmore 86-73.

Mechi mbili za marudiano zitaandaliwa katika ukumbi wa Makande, Mombasa, Jumamosi. Timu zote zilitoka 18-18 na baadaye Bandari ikaongoza 40-38 kipindi cha kwanza kilipomalizika.

Zetech Titans na Chuo Kikuu cha Africa Nazarene zilitoka nyuma na kutoka nguvu sawa 1-1 dhidi ya Terrorists ya Chuo Kikuu cha Nairobi na Pirates ya Chuo Kikuu cha Kenyatta katika robo-fainali ya ligi ya wanaume daraja ya kwanza.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi wa Ruiru waandama wakilalama kuhusu barabara mbovu

Sonko atetea hatua yake kuwasimamisha kazi baadhi ya maafisa

adminleo