• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Kabuu awabwaga wapinzani  Milan Marathon

Kabuu awabwaga wapinzani Milan Marathon

Na GEOFFREY ANENE

MALKIA wa Delhi Half Marathon mwaka 2011, Lucy Kabuu ndiye mshindi mpya wa mbio za Milan Marathon baada ya kunyakua taji nchini Italia, Jumapili.

Kabuu, ambaye alishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2006, alitawazwa bingwa mjini Milan baada ya kukamilisha mbio hizi za kilomita 42 kwa saa 2:27:02.

Aliongoza Wakenya wenzake Vivian Jerono, Sheila Chepkech na Doris Changeywo kufagia nafasi nne za kwanza, mtawalia.

Taji la wanaume lilinyakuliwa na Muethiopia Abdiwak Seifu aliyetumia saa 2:09:04. Wakenya Justus Kimutai (2:10:00) na Barnabas Kiptum (2:10:17) waliridhika katika nafasi ya pili na tatu, mtawalia.

Ushindi wa Kabuu unaendeleza utawala wa Wakenya katika mbio za Milan Marathon za wanawake hadi miaka saba. Seifu naye alikatiza utawala wa wanaume wa Kenya katika Milan Marathon uliokuwa umedumu miaka minne.

Matokeo ya 10-bora (Aprili 8, 2018):

Wanawake

Lucy Kabuu (Kenya) saa 2:27:02

Vivian Jerono (Kenya) 2:27:08

Sheila Chepkech (Kenya) 2:29:26

Doris Changeywo (Kenya) 2:29:50

Fatna Maraoui (Italia) 2:33:18

Elena Loyo (Uhispania) 2:33:20

Laura Gotti (Italia) 2:33:22

Sarah Giomi (Italia) 2:42:32

Laura Biagetti (Italia) 2:46:51

Claudia Marietta (Italia) 2:59:08

 

Wanaume

Abdiwak Seifu (Ethiopia) saa 2:09:04

Justus Kimutai (Kenya) 2:10:00

Barnabas Kiptum (Kenya) 2:10:17

Fred Musobo (Uganda) 2:13:50

Camilo Santiago (Uhispania) 2:13:56

Yassine Rachik (Italia) 2:14:01

Abdi Kebede (Ethiopia) 2:14:08

Erik Kering (Kenya) 2:15:13

Elijah Serem (Kenya) 2:15:37

Francesco Bona (Italia) 2:16:16

You can share this post!

Ingwe yaponea kichapo

Starlets waingia mkondo wa pili kufuzu Kombe la Afrika

adminleo