• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:12 PM
Chelsea yafuzu baada ya kunyanyasa Forest

Chelsea yafuzu baada ya kunyanyasa Forest

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

MABAO mawili dhidi ya Nottingham Forest katika kipindi cha kwanza kutoka kwa Callum Hudson-Odoi na Ross Barkley, Jumapili usiku yalitosha kuipa Chelsea ushindi wa kusonga mbele katika michuano ya kuwania ubingwa wa FA Cup.

Mbali na kufunga bao la kwanza, kinda Odoi kadhalika alichangia katika kupatikana kwa bao la pili, mbali na kuwaandalia wenzake pasi za uhakika, hasa Michy Batshuayi.

Kulikuwa na utata katika mechi hiyo, na ilibidi mtambo wa VAR utumike kumsaidia mwamuzi ambaye alikuwa amewapa Forest penalti kwa madai kwamba mshambuliaji Alexander Mighton alikuwa ameangushwa na Fikayo Timori katika eneo la hatari, uamuzi ambao ulikataliwa na mtambo huo ulioonyesha kwamba kabla ya kitendo hicho, mchezaji wa Forest alikuwa ameotea.

Mechi hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa klabu ya Chelsea ambayo inasherehekea miaka 50 tangu inyakue ubingwa wa taji hilo kwa mara ya kwanza mnamo 1970 chini ya Dave Sexton.

Jumapili, wachezaji wa Chelsea walivalia mavazi maalum yaliyovaliwa siku wakitwaa ubingwa kwa mara ya kwanza. Ni mechi ambayo ilihudhuriwa na jamaa na baadhi ya mastaa waliokuwa kikosini siku hiyo.

Timu zote zifanya mabadiliko tisa kutoka kwa vikozi vilivyocheza mechi zao za ligi kuu wakati wa Krismasi na Mwaka Mpya.

Nimechi ambayo mashabiki wa Chelsea watamkumbuka Hudson-Odoi ambaye alionyesha kiwango cha juu zaidi, huku akishirikiana na vyema na kinda mwenzake Reece James.

Kombora kali

Pedro aliachilia kombora kali ambalo kwa bahati mbaya lilimpiga Batshuayi na kutoka nje. Katika juhudi za kutafuta bao, Barkley alifunga bao la pili baada ya kombora la Hudson-Odoi kumchanganya kipa Jordan Smith.

Muda mfupi kabla ya wakati wa mapumziko, James na Batshuayi walishirikiana vyema, lakini hawakufanikiwa kuona lango.

Mechi ilipofikia katikati mwa kipindi cha pili, Forest walipata bao kupitia kwa Ryan Yates lakini likakataliwa kwa kuwa alikuwa ameotea.

Kwa mara nyingine mtambo wa VAR ulitumika kubaini ukweli.

Tariq Lamptey aliyeingia katika kipindi cha pili alicheza vizuri kuliko alivyokuwa katika Arsenal. Kinda huyo alichukuwa nafasi ya Pedro na kuzua mashambuliaji makali lengoni mwa Forest, huku akimpa wakati mgumu beki wa kimataifa Michael Dawson.

  • Tags

You can share this post!

SURA TISHO: Liverpool yaicharaza Everton 1-0 dimba la FA

Washukiwa wawili wa al-Shabaab waliovamia kituo wauawa...

adminleo