• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
City Stars yazidi kutetemesha BNSL

City Stars yazidi kutetemesha BNSL

Na JOHN KIMWERE

WANASOKA wa Nairobi City Stars waliendelea kufyeka wapinzani wao kwenye kampeni za kuwania taji la Betika Supa Ligi ya Taifa (BNSL) walipochapa Shabana FC bao 1-0 uwanjani Gusii Stadium mjini Kisii.

Nayo Bidco United ilikandamiza Mt Kenya United kwa magoli 5-2 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye jedwali kwa alama 39 huku Muranga Seal ikibeba mabao 2-1 mbele ya Kibera Black Stars.

City Stars ambayo hunolewa na kocha, Sanjin Alagin ilipata mtihani mgumu mbele ya wenyeji wao kabla ya Abdallah ‘Shittu’ Salim kufanya kweli.

Mshambuliaji huyo alifanikiwa kutikisa wavu mara moja na kubeba City Stars kutia kapuni alama tatu muhimu.

”Bila shaka mchezo huo haukuwa mteremko lakini nashuruku vijana wangu waliojituma mithili ya mchwa na kufanikiwa kujiongezea pointi zote,” alisema kocha huyo wa City Stars.

Vilevile alipongeza wasajili wapya Peter ‘Pinchez’ Opiyo na Aziz Okaka zamani akipigia AFC Leopards kwa kuonyesha soka ya kuvutia kwenye patashika hiyo.

Kocha huyo alisema wanatazamia kutaja wachezaji wanne wapya wanapania kusajili baada ya kukamilisha kujadiliana nao.

City Stars inaonekana imekaa vizuri huku ikijivunia kufanya usajili wa nguvu mwanzoni mwa kipute cha muhula huu.

Kwenye mfululizo wa matokeo hayo, Ushuru FC ya kocha, James ‘Odijo’ Omondi ilijiongezea pointi moja baada ya kuagana sare ya bao 1-1 na St Josephs Youth.

Nao wachana nyavu wa Coast Stima walirejea makwao wakinuna baada ya kulimwa mabao 2-1 na wenyeji wao Fortune Sacco.

City Stars ingali kifua mbele kwenye jedwali kwa alama 46 baada ya kushuka dimbani mara 19 ambapo imesajili ushindi wa mechi 14, kutoka nguvu sawa mara nne na kudondosha patashika moja iliponyukwa bao 1-0 na Kibera Black Stars (KBS).

You can share this post!

KSG Ogopa wabanwa na South C United

Mwanasoka atia saini kucheza hadi umri wa miaka 53

adminleo