• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Homeboyz yaendelea kuonyesha ni mgombea halisi wa taji

Homeboyz yaendelea kuonyesha ni mgombea halisi wa taji

Na GEOFFREY ANENE

BAADA ya kusikitisha kwenye Ligi Kuu ya raga nchini (Kenya Cup) kwa kumaliza msimu uliopita katika nafasi ya tisa, Homeboyz imeendelea kuonyesha ni mgombea halisi wa taji msimu huu wa 2019-2020 ilipolipua mabingwa wa zamani Kenya Harlequin 48-3 uwanjani RFUEA, Jumamosi.

‘Madeejay’ hao walivuna ushindi huo muhimu kupitia miguso ya Bob Muhati (miwili), Zeden Marrow, Joshua Chisanga, Stanley Isogol, Meshach Akenga na Leonard Mugaisi, huku Mohamed Omollo na Ervin Asena wakichangia mikwaju mitano. Omollo pia alifunga penalti katika mechi hiyo ya raundi ya 12. Wenyeji Quins walijiliwaza na penalti kutoka kwa Lyle Asiligwa.

Viongozi Kabras Sugar waliedelea kuonyesha ubabe wao dhidi ya Kisumu kwa kuwapepeta 59-13 mjini Kisumu. Wanasukari wa Kabras walikuwa wameaibisha Kisumu 89-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza mjini Kakamega.

Mabingwa watetezi KCB, ambao Ijumaa usiku walitawazwa washindi wa timu bora ya mwaka nchini Kenya katika tuzo ya SOYA mjini Mombasa, pia walizidi kutesa ligini na kuwekea presha Kabras kwa kucharaza Western Bulls 29-8 mjini Kakamega.

Nao majirani Nakuru na Menengai Oilers walitoana jasho mjini Nakuru kabla ya wenyeji Nakuru kuponyoka na ushindi mwembamba wa alama 19-17.

Mabingwa wa zamani Mwamba pia walitolewa kijasho chembamba nyumbani baada ya kuongoza 15-0 kabla ya kushinda Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta 15-14.

Impala Saracens pia walikuwa na siku nzuri hapo jana walipohangaisha washikilizi wa rekodi ya mataji mengi ya ligi, Nondescripts, na kuwapiga 28-18.

You can share this post!

Umoja wa Nasa ‘wafufuka’ katika mkutano wa BBI...

Wandani wa Ruto wamrai Rais Uhuru asimteme

adminleo