• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
ULIMBWENDE: Tumia viazi kulainisha ngozi

ULIMBWENDE: Tumia viazi kulainisha ngozi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

VIAZI vina madini muhimu kama vitamini A, B, C na chuma na pia vina manufaa kwa ngozi yetu.

Unaweza kutumia viazi nyumbani ili kuwa na ngozi nyororo.

Faida za viazi kwa ngozi

Viazi huondoa madhara yaliyosababishwa na jua na kuleta mwanga wa asili wa ngozi.

Viazi inapunguza uwekundu na matatizo ya ngozi kutokana na vipele ,makovu na chunusi.

Viazi vinafanya ngozi iwe rangi moja na laini.

Viazi husaidia kuondoa mikunjo kwenye uso

Viazi huondoa weusi kwapani

Husaidia ngozi iwe na rangi moja.

Utahitaji

  • vijiko vitatu vya juisi ya viazi
  • mafuta ya lozi vijiko viwili (almond oil)
  • maziwa vijiko viwili

Cha kufanya

Kwenye kibakuli changanya mahitaji yote na upake kwenye uso bila ya kusahau shingo na sehemu zote utakazohitaji.

Iache kwa dakika 30 kisha osha kwa maji fufutende.

Kuondoa makovu na madoa

Mahitaji

  • kipande cha kiazi
  • sukari vijiko 2

Cha kufanya

Nyunyiza sukari kidogo kwenye kipande cha kiazi na ujisugue kwa dakika tano.

Uache mchanganyiko kwenye uso wako kwa dakika 10 kisha osha kwa maji ya baridi.

Limau na viazi vinatumika kama mkorogo wa asili na huondoa weusi wowote na madoa kwenye ngozi.

Mahitaji

  • kiazi kidogo kimoja kilichopondwa
  • vijiko vitatu vya juisi ya ndimu au limau

Cha kufanya

Ponda kiazi na eka vijiko vitatu vya juisi ya limau

Changanya na paka kwenye makovu

Iache kama dakika 20 mpaka 30 kisha osha vizuri na maji

 

Kwa ngozi iliyoungua kutokana na jua

Maji ya viazi yatasaidia ngozi yako

Mahitaji

  • vijiko viwili vya juisi/maji ya viazi
  • kijiko kimoja cha asali

Cha kufanya

Changanya bidhaa zote unazohitaji pamoja na upake kwenye uso.

Ache kama dakika 15 kisha osha.

Kausha vizuri na paka losheni au mafuta unayopenda.

Kwa kuondoa mikunjo

Viazi huondoa na kupunguza mikunjo kwenye uso

Mahitaji

  • kiazi kimoja kilichopondwa
  • vijiko viwili vya maziwa
  • glycerine kiasi

Cha kufanya

Katika bakuli tia kiazi kilichopondwa na maziwa, changanya vizuri.

Ongeza gycrerine na changanya.

Paka mchanganyiko kwenye uso wako na uache kama dakika 15.

Osha kwa maji fufutende kisha ufute uso.

You can share this post!

Nchi kadha zapinga mpango wa Trump kuhusu Palestina

James Nyoro atarajiwa kuapishwa Gavana mpya wa Kiambu

adminleo