• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 8:55 AM
Tundo afungua mwanya wa alama tano katika mbio za magari Kenya

Tundo afungua mwanya wa alama tano katika mbio za magari Kenya

Na MWANDISHI WETU

DEREVA Carl “Flash” Tundo amechukua uongozi wa mapema wa Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) 2020, baada ya kujizolea alama 25 kwa kushinda duru ya ufunguzi ya KCB Guru Nanak katika maeneo ya Stoni Athi, Jumapili.

Katika mfumo mpya wa kupatia washiriki pointi, Tundo, ambaye alifanikiwa kutetea ubingwa wake wa Guru Nanak kwa mara ya pili mfululizo, aliongezwa alama tatu za bonasi.

Baldev Chager, ambaye aliibuka mfalme wa mbio za magari nchini mwaka 2019, alikusanya alama 21 kwa kumaliza nyuma ya Tundo. Chager pia alitunukiwa alama mbili za bonasi na sasa ana jumla ya alama 23.

Onkar Rai anakamilisha orodha ya madereva tatu-bora waliopokea alama za bonasi.

Onkar alitia kapuni alama 18 kwa kukamilisha Guru Nanak katika nafasi ya tatu na kuambulia alama moja ya bonasi.

Tundo na Chager waliendesha magari ya Mitsubishi EvoX naye Onkar akatumia VW Polo.

Ian Duncan (Nissan Patrol), Jasmeet Chana (Mitsubishi EvoX), Nikhil Sachania (Mitsubishi EvoX) na Evans Kavisi (Subaru Impreza), ambao walifuatana kutoka nafasi ya nne hadi saba wamezoa alama 15, 12, 10 na nane, mtawalia.

Duru ya pili itaandaliwa katika kaunti ya Nakuru wikendi ya Machi 8-9.

Onkar anatarajiwa kutetea ubingwa wa Nakuru Rally baada ya kutawala makala ya mwaka 2017, 2018 na 2019.

  • Tags

You can share this post!

Tusker sasa yainuka Gor na Ingwe wakijikwaa Ligi Kuu

Maafisa wanne wakamatwa kwa kuvamia makazi ya Midiwo

adminleo