• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Kenya yataja mabondia 13 watakaowania tiketi za kushiriki Olimpiki

Kenya yataja mabondia 13 watakaowania tiketi za kushiriki Olimpiki

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imetaja kikosi chake cha mabondia 13 watakaowania tiketi za kushiriki Michezo ya Olimpiki 2020 kutoka kwa mchujo wa Bara Afrika utakaoandaliwa jijini Dakar nchini Senegal mnamo Februari 20-29.

Mabingwa wa uzani wa kati wa ndondi za kulipwa za Bara Afrika (ABU) Rayton Okwiri,33, ambaye alishiriki Olimpiki 2016 mjini Rio de Janeiro nchini Brazil baada ya kushinda mchujo wa Afrika katika uzani wa kilo 69 (Welter) nchini Cameroon, atajaribu bahati tena, ingawa katika uzani tofauti ule wa kilo 75 (Middle) mjini Dakar.

Hassan Shaffi Bakari ambaye alishinda medali ya fedha ya uzani wa kilo 52 (Flyweight) katika michezo ya Afrika (African Games) nchini Morocco mwaka 2019 pamoja na Elly Ajowi na Fredrick Ramogi walionyakua medali za shaba katika michezo hiyo mjini Rabat katika vitengo vya uzani wa kilo 91 (Heavy) na zaidi ya kilo 91 (Super Heavy) mtawalia, pia wako katika orodha hiyo ya mabondia wanane wanaume na wanawake watano. Kikosi cha kilichoanza matayarisho kilijumuisha mabondia 28 kabla ya kuchujwa. Timu hiyo imekuwa chini ya kocha Benjamin Musa kambini mjini Nanyuki. Imeratibiwa kusafiri nchini Senegal mnamo Februari 17.

Kikosi cha Kenya:

Wanaume

Nick Okoth (Featherweight)

Rayton Okwiri (Middleweight)

Hassan Shaffi Bakari (Flyweight)

Elly Ajowi (Heavyweight)

Joseph Shigali (Lightweight)

Boniface Mugunde (Welterweight)

Humphrey Ochieng’ (Light Heavyweight)

Fredrick Ramogi (Super Heavyweight)

 

Wanawake

Elizabeth Andiego (Middleweight)

Christine Ongare (Flyweight)

Evelyne Akinyi (Lightweight)

Elizabeth Akinyi (Welterweight)

Beatrice Akoth (Featherweight)

You can share this post!

MBOGA YAJA: Liverpool yazuru Carrow Road kukabiliana na...

Hafla ya kumuenzi Mzee Maulidi Juma yafana mjini Mombasa

adminleo