• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Harambee Starlets yapata mwaliko Uturuki kumenyana na mataifa kadhaa

Harambee Starlets yapata mwaliko Uturuki kumenyana na mataifa kadhaa

Na GEOFFREY ANENE

MABINGWA wa soka ya wanawake ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Harambee Starlets wamepata mwaliko kuwania ubingwa wa dimba la Turkish Women Cup mnamo Machi 2-11, 2020.

Dimba hilo litaleta pamoja Uturuki, Kenya, Hungary, Venezuela, Hong Kong, Romania, Uzbekistan, Northern Ireland, Turkmenistan na Chile.

Kocha David Ouma anatarajiwa kutangaza kikosi cha kuanza mazoezi hapo Februari 19. Starlets, ambayo imeratibiwa kuanza matayarisho hapo Februari 23 jijini Nairobi, itatumia dimba hilo kujipiga msasa kabla ya mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AWCO ) 2020 kuanzia mwezi Aprili.

Vipusa wa Ouma watapimana nguvu dhidi ya timu ya humu nchini Februari 29 kabla ya kuelekea Uturuki mnamo Machi 2.

“Nafurahi sana Starlets imetambulika na kualikwa kushiriki mashindano ya kimataifa nchini Uturuki. Michuano hiyo itatupatia fursa nzuri ya kupima wachezaji wetu kabla ya mechi za kuingia AWCON kuanza,” alisema Ouma.

Mashindano ya Uturuki pia yanapatia mshambuliaji mpya wa Besiktas Esse Akida fursa nzuri ya kurejea katika kikosi cha Starlets.

Akida, ambaye alinunuliwa na Besiktas mnamo Februari 17 kutoka nchini Israel, alichezea Starlets mara ya mwisho mwaka 2018.

Besiktas inapatikana jijini Istanbul nchini Uturuki.

You can share this post!

Mudavadi alitaka jopo la BBI kuhakikishia Wakenya ripoti...

Mama asema polisi wanachunguza kisa cha mtoto wa umri wa...

adminleo