Rais amlipia faini aliyetupwa ndani kwa kusafirisha nyoka bila kibali
Na WINNIE ATIENO
MWANAMUME aliyefungwa miaka miwili jela kwa kumiliki nyoka bila kibali ameachiliwa kutoka Shimo la Tewa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kumlipia faini ya Sh1 milioni.
Benedict Karisa Iha alikuwa amefungwa jela baada ya kukosa kulipa faini ya Sh1 milioni.
Aliachiliwa kutoka kwa gereza la Shimo la Tewa Februari 20.
Bw Karisa amesema alikuwa gerezani alipoitwa na askari jela waliomuambia alikuwa na wageni waliotaka kumuona.
“Wageni wangu walikuwa ni OCPD wa Mombasa OCPD akiwa na kamanda wa gereza, ambapo OCPD alinieleza nilifaa kupelekwa kwa mshirikishi wa kanda ya pwani John Elungata ambapo familia yangu ilinisubiri. Nilifika na nikaambiwa Rais Uhuru Kenyatta alikuwa amenilipia faini,” amesema Bw Karisa.
Bw Elungata alimpa Sh8340 kama nauli ya kurudi nyumbani.
Amesema ameahidiwa pesa za kuanzisha biashara ajiepushe na kusafirisha nyoka.
Anadai ana kibali ila siku ya kosa alikuwa amesahau kukibeba alipokamatwa katika kivuko cha Likoni akiwa na nyoka mwenye urefu wa mita 2.3 na akiwa na uzani wa kilo 10 akiwa amemfungia katika kitambaa ndani ya pakacha akisafirisha kuelekea Ukunda, Diani, Kaunti ya Kwale.
Narrating his ordeal to Nation during an exclusive interview at their Mtwapa home, Mr Karisa said he was called by his father to go and fetch a snake from Mtwapa and take it to Diani.
Anasema alijifunza ‘kazi’ hiyo kutoka kwa babake.