Spurs yalenga kuondoa rekodi duni gozi la Uefa
Na MASHIRIKA
LEIPZIG, Ujerumani
TOTTENHAM Hotspur watashuka dimbani hii leo Jumanne nchini Ujerumani kuvaana na RB Leipzig, katika mchuano wa mkondo wa pili wa hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (Uefa).
Vijana wa kocha Jose Mourinho wanalenga kubatilisha kichapo cha 1-0 walichopewa na Leipzig jijini London, Uingereza mnamo Februari 19.
Fauka ya hayo, kibarua cha leo kitakuwa kigumu zaidi kwa Tottenham ambao wamepoteza mechi saba kati ya 14 zilizopita dhidi ya mpinzani kutoka Ujerumani.
Penalti ya Timo Werner katika mechi ya raundi ya kwanza ilididimiza zaidi matumaini ya Tottenham, ambao sasa watalazimika kujitahidi maradufu ili kuweka hai matumaini yao ya kutinga robo-fainali.
Japo Leipzig si miongoni mwa vikosi vinavyopigiwa upatu wa kutawazwa wafalme wa UEFA msimu huu, kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kimepania kuwaangusha Tottenham.
Kufikia sasa, Leipzig wanashikilia nafasi ya pili katika Bundesliga kwa alama 50 kutokana na mechi 25.
Isitoshe, hawajapoteza mechi yoyote kati ya sita zilizopita katika mapambano yote. Kibarua cha mwisho cha ligi kwa kikosi hicho cha kocha Julian Nagelsmann, kiliwashuhudia wakitoka sare tasa dhidi ya VfL Wolfsburg ugenini.
Ingawa hivyo, nafuu zaidi kwa Tottenham ni rekodi mbovu ya Leipzig katika mechi za UEFA nyumbani.
Wameibuka na ushindi mara moja pekee kutokana na mechi nne zilizopita mbele ya mashabiki wao nyumbani.
Akihojiwa wikendi, kocha Nagelsmann alidokeza uwezekano wa kudumisha kikosi alichokitegemea katika mkondo wa kwanza.
Safu ya mbele itasalia kuongozwa na Werner, ambaye anahusishwa pakubwa na Liverpool.
Nyota huyo anajivunia mabao 27 katika mechi 42 za mapambano yote kufikia sasa.
Kwa upande wao, Tottenham watajibwaga ugani wakiwa na kiu ya kujinyanyua baada ya kutosajili ushindi wowote katika mechi tano zilizopita.
Katika michuano hiyo, wamepepetwa mara nne kwenye mashindano matatu tofauti.
Lucas Moura, Harry Winks, Serge Aurier na Giovani Lo Celso wanatazamiwa kuunda kikosi cha kwanza, kitakachokosa huduma za Juan Foyth, Steven Bergwijn, Moussa Sissoko, Harry Kane na Son Heung-min.
Katika mechi nyingine, Valencia wataalika Atalanta wakiwa lazima wasajili ushindi wa 3-0 ili kusonga mbele. Miamba hao wa Uhispania walidunguliwa 4-1 na Atalanta katika mkondo wa kwanza nchini Italia.
RATIBA YA UEFA
Leo: Leipzig na Tottenham
Valencia na Atalanta
Kesho: PSG na Dortmund
Liverpool na Atletico
Walijizolea alama moja dhidi ya Burnley katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wikendi, baada ya kuzidiwa maarifa katika mechi mbili kati ya tatu za awali.
Matokeo hayo yaliwafanyaa kushuka hadi nafasi ya nane katika EPL wakiwa na pointi 41, saba nyuma ya Chelsea wanaofunga mduara wa nne-bora.
Licha ya kupoteza mechi za makundi dhidi ya Bayern Munich, Tottenham walifaulu kusonga mbele katika kipute cha UEFA muhula huu. Walitinga fainali iliyowakutanisha na Liverpool msimu uliopita baada ya kuwalaza Borussia Dortmund, Man-City na Ajax katika hatua za mwisho za gozi hilo.
Ilivyo, kibarua cha leo kitakuwa kigumu zaidi kwa Tottenham ambao wamepoteza mechi saba kati ya 14 zilizopita za soka ya bara Ulaya dhidi ya mpinzani kutoka Ujerumani.
Lucas Moura, Harry Winks, Serge Aurier na Giovani Lo Celso waliokuwa wachezaji wa akiba dhidi ya Burnley wanatazamiwa kuunga kikosi cha kwanza cha Tottenham kitakachokosa huduma za Juan Foyth, Steven Bergwijn, Moussa Sissoko, Harry Kane na Son Heung-min.
RATIBA YA UEFA (Leo):
Leipzig na Tottenham
Valencia na Atalanta
(Kesho Jumatano):
PSG na Dortmund
Liverpool na Atletico
Mchuano wa mkondo wa kwanza ulikuwa wa kwanza kuwahi kukutanisha kikosi cha soka ya Ujerumani na Tottenham katika historia ya mashindano ya UEFA. Pia ilikuwa mara ya kwanza kwa Leipzig kuonja makali ya klabu inayonogesha kabumbu ya Uingereza.
ha UEFA msimu huu, Leipzig walikamilisha kampeni za Kundi G wakijivunia alama tatu zaidi kileleni, na kwa sasa wanajivunia kusajili ushindi kutokana na mechi sita kati ya 13 zilizopita za bara Ulaya.