Michezo

Euro yaahirishwa hadi 2021 kuzuia athari za corona

March 19th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MASHIRIKA

SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA) sasa limekiri kuahirisha mashindano ya Euro 2020 hadi mwaka ujao ili kuwa na muda wa kutosha kwa Ligi ya Premier na mashindano mengine ya barani Ulaya kumalizika baada ya kutokea kwa janga la Corona.

Virusi vya Corona vyaendelea kuzua hofu, kiasi cha kuwaacha wanamichezo katika nyakati zisizo za kawaida.

Mlipuko wa virusi vya Corona umesababisha michezo mingi tu kufutiliwa mbali nchini Uingereza na kote duniani ikiwemo katika mchezo wa soka Uingereza.

Janga hili limesababisha mechi nyingi kote duniani kufutiliwa mbali ndani ya saa 24.

Ijumaa, ligi ya Premier ilikuwa ndiyo moja ya mashindano ya mpira wa soka mashabiki walikuwa wanasubiri hatma yake baada ya mkutano wa dharura kuitishwa.

Matokeo yake ligi ya Premier na EFL ikatangaza kwamba hakuna tena michuano ya mpira wa soka mpaka Aprili.

Ukweli ni kwamba hakutakuwa na michezo yoyote ya mpira wa soka Uingereza katika kipindi cha wiki tatu zijazo huku mwanahabari wa BBC akisema kwamba kurejelewa kwa ligi ya Premier League na EFL 3-4 Aprili ni jambo ambalo lisilokuwa na uhakika.

Mchuano pekee ya soka uliokuwa umepangwa wikendi hii ulikuwa ni baina ya Wales na Scotland, lakini ukaahirishwa

Pia ikatangazwa kwamba mashindano ya London Marathon yaliyokuwa yafanyike Aprili yameahirishwa hadi Oktoba.