Habari

CORONA: Naibu Gavana na padre walivyoeneza virusi hatari

March 24th, 2020 Kusoma ni dakika: 2

MOHAMED AHMED NA MAUREEN ONGALA

ATHARI za tabia ya Naibu Gavana wa Kilifi Gideon Saburi ya kutangamana na watu badala ya kujitenga baada ya kurudi nchini kutoka Ujerumani, zimeanza kuonekana, baada ya baadhi ya watu aliokutana nao kuanza kuugua.

Bw Saburi ametengwa na serikali hospitalini kwa lazima. Wasiwasi pia umetanda katika Kaunti ya Siaya baada ya padre aliyekuwa amesafiri Roma nchini Italia kuthibitishwa anaugua virusi vya corona.

Padre huyo aliporudi nchini hakujitenga ilivyoagizwa na serikali, na badala yake aliendelea na shughuli za kanisa ikiwemo kuongoza ibada na mazishi.

Mapadre wenzake wapatao 100 na watawa 30 wanaishi kwa hofu kwani wal- ipokea sakramenti kutoka kwake.

Katika kisa cha Bw Saburi, Taifa Leo ilithibitisha kuwa maafisa wawili wakuu wa polisi wa kituo cha Mtwapa wametengwa baada ya kupata matatizo ya kupumua, ambayo ni moja ya dalili za virusi vya corona Wawili hao ni Naibu OCS wa Mtwapa Benard Otomei na kamanda wa trafiki Mathew Koech, ambao walikutana na Bw Saburi katika eneo moja la burudani mjini Mtwapa.

Ripoti ya polisi ilieleza kuwa Bw Otomei alikuwa akilalamika kuwa na shida ya ku- pumua, jambo lililomlazimu yeye na Bw Koech kujitenga wakisubiri majibu ya vip- imo vya matibabu.

“Tunasubiri majibu ya uchunguzi wa sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa maafisa wa afya ya umma kutoka Kilifi,” ilisema ripoti ya polisi.

Afisa mmoja wa ngazi za juu alithibit- ishia Taifa Leo kuwa maafisa hao na Bw Saburi walikuwa pamoja wakijiburudisha Mtwapa.

Bw Saburi alitoka jijini Berlin, Ujerumani mnamo Machi 6 na badala ya kujitenga akaungana na maafisa wakuu wa kaunti na wananchi wa kawaida.

Mnamo Machi 8 alihudhuria hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawale katika eneo la Rabai, kwenye hafla ambayo ilihudhuriwa pia na Mbunge Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu, Mbunge wa Rabai Wil- liam Kamoti na Waziri Msaidizi wa Wiz- ara ya Ardhi Gideon Mung’aro.

Bw Kamoti jana asubuhi alilazwa katika hospitali moja ya kibinafsi eneo la Nyali baada ya kupata matatizo ya kupumua. Gavana Amason Kingi alijitenga mnamo Machi 19 baada ya kukutana na naibu wake, na akawatuma maafisa wa afya kuatafuta watu wote waliotangamana na Bw Saburi.

Habari za baadhi ya watu aliokutana nao kuwa na matatizo ya kupumua zi- najiri huku mwenyekiti wa Kenn Trade Suleiman Shahbal akitangaza kuwa hata yeye amejitenga, kwa kuwa alikutana na Gavana Kingi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Moi, mjini Mombasa mnamo Alhamisi iliyopita.

“Kama ambavyo Gavana Kingi ameenda kujitenga, mimi pia najitenga mara mojakwa siku 14,” akaandika  Shahbal kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Jana, Mbunge wa malindi Aisha Jumwa alisema tabia ya Bw Saburi imeibua taharuki Kilifi baada ya kubainika kuwa huenda amewaambukiza watu wengi virusi vya corona.

Naibu Kamishna wa Kaunti wa Kilifi Kaskazini Josephat Mutisya, alisema af- isi yake inashirikiana na idara ya afya ya kaunti kuwasaka wote waliokutana na Bw Saburi.

Wasiwasi pia ulitanda awali kuwa huenda Kiongozi wa chama cha ODM, Rai- la Odinga alikutana na Bw Saburi, jambo ambalo afisi yake ilikanusha jana.

Msemaji wake Dennis Onyango, alisema ijapokuwa Bw Odinga alikuwa katika ziara ya kibinafsi eneo la Pwani wiki iliyo- pita, alikutana na Naibu Gavana wa Mombasa William Kingi pekee wala hakuonana na Bw Saburi.

“Bw Odinga alipozuru Mombasa haku- kutana na viongozi wengine wa Pwani isipokuwa Naibu Gavana wa Mombasa William Kingi. Hakukutana na Bw Saburi wala kiongozi mwingine yeyote,” ikasema taarifa kutoka ofisi ya Bw Odinga.

Taarifa hiyo ilisema Bw Odinga anazingatia kanuni zote zilizowekwa na serikali ikiwemo kuepuka kukutana na watu wen- gi, na ndiposa anafanyia kazi nyumbani.