Mtambo wa kunawia mikono bila kubonyeza
NA DIANA MUTHEU
VIJANA wawili katika kaunti ya Mom- basa wamevumbua mbinu mpya ya kuna- wa mikono bila ya kufungua au kubonyeza mfereji kama njia moja ya kuzuia maam- bukizi ya virusi vya corona.
Unawaji mikono ulikuwa umepuuzwa kwa muda mrefu hadi pale mlipuko wa virusi hivi ulitokea. Ueneaji wa maradhi ya COVID-19 ukiendelea kwa kasi sana ulimwenguni kote, njia moja ya kujikinga ni kudumisha usafi kwa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.
Kenya ikiendelea kujikakamua kupam- bana na virusi hivi, wavumbuzi wawili, Simon Wafula, 27 na Edwin Amwoka, 25 kupitia kwa kifaa chao cha kunawia mikono kinachoitwa ‘Automatic Hand Washer’, wanasema kuwa mashine hiyo itawasaidia watu wengi kunawa bila ya kugusa mifereji.
“Kunawa mikono ni jambo muhimu sana haswa msimu ambapo tunapamba- na na virusi vya corona. Tunaona ni sala- ma sana kutumia kifaa hiki cha kunawia mikono kwa kuwa mtu hafungui wala kubonyeza mahali popote kwenye mfere- ji,” akasema Bw Amwoka.
Kifaa hiki cha ‘Automatic Hand Wash- er’ kinatumika pamoja na tanki ya maji (au maji katika ndoo), chupa ya sabuni na dispensa (kifaa kinachoning’iniza vitu kama vile maji, sabuni) ambapo upande mmoja kuna sabuni na huo mwingine maji.
Ndipo dispensa hiyo ifanye kazi ipasavyo, mtu anafaa kuweka mkono chini yake ama kwa upande wa maji au sabuni. Dispensa hii ina kidude ambacho kinaweza kufahamu kuwa mtu ameweka mkono, ndipo kikafungulia sabuni hiyo au maji.
Pia, maagizo yamewekwa kwenye mashine hiyo kuonyesha maji au sabuni yanatokea wapi.
“Kila mtu kwa sasa anajaribu asiguse uso wake, vyuma, mbao na sehemu tofau- ti zinazotuzingira kama njia ya kujiepu- sha na maambukizi ya virusi hivi. Mfereji kama huu ambao mtu hahitaji kuugusa ni salama,” akasema Bw Wafula.
Wawili hawa ambao walihitimu na sha- hada ya Uhandisi katika Umeme kutoka Chuo cha Ufundi cha Mombasa (TUM), walisema kuwa mtambo huu unaweza ku- tumia kawi ya aina mbali mbali.
“Inaweza kutumia umeme, kawi ya jua au betri. Maazimio yetu yalikuwa kuhakikisha kuwa hata walio mashambani ambako hakuna umeme wanaweza pia kuutumia mtambo huu,” akasema Wafula.
Wavumbuzi hawa wanaofanya kazi katika kampuni moja ya kuuza vifaa vya kawi ya jua walisema washafanya jaribio na mashine hii inafanya kazi ipasavyo.