Habari

CORONA: Nairobi na Pwani hatarini zaidi

March 25th, 2020 Kusoma ni dakika: 3

NA WAANDISHI WETU

KENYA sasa ina wagonjwa 25 wa virusi vya corona baada ya waziri wa Afya Bw Mutahi Kagwe kutangaza visa vingine 9 hapo Jumanne.

Wagonjwa ambao walithibitishwa kuugua ugonjwa huo walipatikana katika kaunti za Mombasa, Kwale na Kilifi ambazo zipo kwenye ufuo wa bahari na hivyo kuvutia watalii wengi, pamoja na Nairobi.

“Tulipokea matokeo ya vipimo 82 ndipo ikathibitishwa watu tisa zaidi wameambukizwa. Hii inafanya idadi ya walioambukizwa corona kuwa watu 25 nchini. Hawa wote wanatoka katika kaunti nne ambazo ni Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale,” akasema Bw Kagwe.

Waziri Kagwe alisema waathiriwa wapya tisa wanajumuisha Wakenya saba, ambapo watatu walipata maradhi hayo kwa kutangamana na watu wengine waliokuwa wametoka nje ya nchi.

“Tunawafuatilia kwa karibu watu 647 waliotangamana na waliothibitishwa kuambukizwa. Kati ya hao, 15 wamelazwa hospitali ya Mbagathi na tunasubiri ma- tokeo ya vipimo vyao,” akasema.

Hapo jana watu wote walioingia nchini kutoka nje walipelekwa moja kwa moja hadi maeneo ya kutengwa kama ilivyo- agizwa na serikali ili kuzuia kuingia kwa watu walio na virusi hivyo nchini.

Tayari virusi hivyo vilivyozuka nchi- ni China mnamo Desemba, 2019, vimethibitishwa kuambukizwa watu zaidi ya elfu 396 kote duniani na elfu 17 kati yao wamefariki.

Hali nchini Italia iliendelea kuwa ya kusikitisha huku idadi ya waliokufa ikika- ribia kuwa maradufu ya waliokufa China.

Kufikia jana watu zaidi ya  6,000 walikuwa wamekufa Italia ikilinganishwa na 3,000 China. Marekani nayo ilipanda katika orodha ya maambukizi hadi nafasi ya tatu baada ya China na Italia ikiandikisha visa 46,000 mbele ya Uhispania (39,000) na Ujerumani (31,000).

Humu nchini, Kaunti ya Kilifi iliendelea kuwa katika hali ya taharuki kutokana na kisa ambapo Naibu Gavana Gideon Sa- buri anashukiwa kuambukiza watu wengi kwa tabia yake ya kutangatanga aliporudi nchini kutoka Ujerumani, badala ya ku- jitenga.

Viongozi kadhaa wa Pwani akiwemo gavana wa Kilifi Amason Kingi, wame- jitenga baada ya kutangamana na Bw Sa- buri ama na watu aliojumuika nao.

Wasiwasi pia umetanda katika kaunti za Siaya na Kisumu ambako Padre Richard Oduor, ambaye amethibitishwa kuu- gua virusi vya corona, alitangamana na watu kadhaa.

Maeneo ambayo Padre huyo alijumuika na watu ni Ugunja, Ambira na Lwak katika Kaunti ya Siaya. Mmoja wa mapadre aliokuwa nao katika mazishi eneo la Ugunj baadaye aliongoza mazishi katika eneo la Muhoroni, Kaunti ya Kisumu mnamo Jumamosi iliyopita, ambako alijumuika na waom- bolezaji kadhaa.

Padre huyo alisema Oduor aliweza ku- jumuika na watu wengi waliochangamkia kurudi kwake nchini kutoka Italia.

Katika Kaunti ya Kilifi, wafanyikazi wote katika idara ya afya walio mapumzikoni na masomoni wameagizwa kurejea kazini mara moja serikali hiyo inapojiandaa kukabiliana na janga la corona iwapo litazuka.

Katibu wa Kaunti Arnold Mkare ame- wapa hadi Jumapili hii wawe wamefika kazini bila kukosa.

“Mfanyikazi yeyote atayekaidi agizo hili bila kutoa sababu ya kueleweka ata- chukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwemo pia kufutwa kazi bila onyo,” akasema Bw Mkare.

Wakati huo huo, vifaa vya kupambana na corona vilivyotolewa na bilionea Jack Ma wa China vilifikishwa nchini jana.

“Leo tumepokea vifaa 20,000 vya kupimia corona kutoka kwa Jack Ma. Nataka kwa niaba ya serikali ya Kenya nimshuku- ru kwa ukarimu wake. Pia nawashukuru Wakenya wengi wanaoisaidia serikali kwa njia mbalimbali,” akasema Bw Kagwe.

Aliwaomba Wakenya waunge mkono juhudi za serikali kukabiliana na maam- bukizi ya virusi vya corona, kwa kutii maagizo waliyopewa, akisema masharti zaidi yatatangazwa leo.

“Watu wote wanaotumia feri wanapaswa kunawa mikono na kutumia vitambaa kufunika midomo na pua. Matatu, tuktuk, bodaboda na wachuuzi katika eneo la mae- gesho la feri wataondolewa ili kupunguza msongamano wa watu.”

Naibu Gavana wa Mombasa William Kingi alisema kuwa kuna baadhi ya watu Momba- sa ambao wameambukizwa virusi vya corona, na sharti watu wazingatie mikakati ili- yowekwa ili kuepuka kusam- baza kwa wenzao.

“Virusi hivi vishatufikia Mombasa. Baadhi ya watu wameambukizwa na wengine zaidi wanashukiwa kuwa navyo. Kati ya visa vingi am- bavyo vipo nchini, wengi wa waathiriwa ni watu wanaoishi Mombasa. Kwa hivyo mambo yatabadilika sasa,” akasema Dkt Kingi.

Aliwaomba wakazi wote wabakie ndani ya nyumba zao, na kwamba sehemu kama vile Likoni, Feri, matatu, mabasi na sehemu za ibada ni hatari sana.

Pia aliwaomba wakazi wote wanawe mikono mara kwa mara wakitumia maji safi na sabuni. Katika kivuko cha feri cha Likoni watu wapatao 320,000 huvuka kila siku.

Serikali imetoa maji na sabuni kwa abiria baada ya mifereji 200 kuwekwa katika pande zote mbili za kivuko hicho ili wazingatie usafi.

Abiria wengi walisema kuwa bado wanasongamana katika feri, hali inayowatia wasiwasi wa maambukizi kuenea.