• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
MWANAMKE MWELEDI: Mtetezi wa haki za Wakenya

MWANAMKE MWELEDI: Mtetezi wa haki za Wakenya

Na PAULINE ONGAJI

Njeri Kabeberi ni mwanaharakati shupavu anayetetea haki za kijamii huku taaluma yake katika nyanja hii ikizidi miaka 20.

Amekuwa akipigania siasa ya kushirikisha watu wote nchini Kenya na katika sehemu zingine, huku akiangazia demokrasia na haki za kibinadamu.

Bi Kabeberi alikuwa katika mstari wa mbele katika vita vya kupigania haki za kibinadamu na demokrasia ya vyama vingi katika miaka ya tisini.

Mwaka wa 1991, alianzisha na kusimamia vuguvugu kwa jina Release Political Prisoners na hatimaye kupelekea kuanzishwa kwa sehemu maalum ya mashujaa wa uhuru yaani Freedom Corner katika bustani ya Uhuru Park in Nairobi.

Alihudumu kama mwanachama wa bodi ya Tume ya haki za kibinadamu kuanzia mwaka wa 1993 hadi 2006 na baadaye, pia kuhudumu katika shirika la Citizen’s Coalition for Constitutional Change.

Kati ya mwaka wa 1997 na 2004, alihudumu kama mratibu wa kimaendeleo wa shirika la Amnesty International, eneo la Afrika Mashariki na Kusini.

Aidha, Bi Kabeberi alianzisha Centre for Multiparty Democracy-Kenya (CMD-K), shirika ambalo limekuwa likinuia kusaidia kuweka muundo wa vyama vya kisiasa kama mbinu ya kuimarisha demokrasia na haki za kibinadamu nchini Kenya.

Alihudumu kama mkurugenzi mtendaji kati ya mwaka wa 2004 na 2009, na alikuwa mratibu wa humu nchini katika shirika la Netherlands Institute for Multiparty Democracy.

Mwanaharakati huyu wa demokrasia na haki za kibinadamu, alitetea kuundwa kwa serikali ya muungano na ushirika wa vyama vya kisiasa. Utetezi wake wa haki za kibindamu umemvunia utambuzi hapa nchini na kimataifa.

Amewahi pokea utambuzi wa Ukanda wa Demokrasia (Democracy Ribbon) kutoka kwa serikali ya Uholanzi, kutokana na vita vyake vya kutetea haki za kibinadamu na demokrasia nchini Kenya. Mwaka wa 2009 alipewa tuzo ya Humanity Award kutoka kwa baraza la mawakili jijini Frankfurt, nchini Germany.

Aidha, aliwahi pokezwa tuzo ya Mau Mau Warriors baada ya kupigania kutambuliwa kwao kutokana na mchango wao katika vita vya kupigania uhuru.

Januari mwaka wa 2008, wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu, jina lake Bi Kabeberi lilichapishwa kwenye orodha ya watetezi wa haki za kibinadamu ambao huenda wangelengwa na kushambuliwa, kwani ilisemekana kwamba kwa mwito wake wa kukomeshwa kwa ghasia ulimaanisha kwamba alikuwa msaliti kwa jamii yake.

Septemba mwaka wa 2016, Bi Kabeberi alitajwa kama mkurugenzi mtendaji wa Greenpeace Africa, shirika la kutetea uhifadhi wa mazingira kimataifa, lililoanzishwa mwaka.

You can share this post!

KAFYU: Walevi wang’ang’ania pombe dakika za...

Mapadre, watawa na waumini 46 wakamatwa kwa kusali kinyume...

adminleo