• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
AKILIMALI: Usanii wa kurembesha mifuko unalipa

AKILIMALI: Usanii wa kurembesha mifuko unalipa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Katika duka la Fundi Nyata kwenye jengo la Prime Plaza mjini Nakuru, Akilimali ilimpata akijishughulisha na kutayarisha vitambaa kadhaa tayari kuvishona.

Mshairi anayependa fesheni na mwandishi wa micheo ya kuigiza, Nikodemus Nyatome,22 anayejulikana sana kama fundi Nyata amejipatia jina kwa ujanibishaji wake wa sanaa ya mifuko ya na viatu.

Mhitimu huyo wa Shahada ya Sanaa ya Ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta anasema kwamba ilimbidi kusomea kozi ya muda katika mtindo na muundo na ndipo alipojifunza kutengeneza nguo.

“Baba yangu ananiunga mkono sana, alinishauri nisomee mtindo wa muundo kwani nilikuwa na wakati mwingi wa bure,” anasema.

Baba yake Bernard Nyatome alikuwa mwigizaji Katika Vioja Mahakamani na Fundi Nyata anakiri kwamba alirithi mapenzi yake ya sanaa kutoka kwake.

‘’Mwaka wa 2017, niliamua kubuni mifuko kwani niliona nafasi ya biashara hii mjini Nakuru ninakoishi. Kabla kujua kutengeneza mifuko, nilimwendea mkiaji ambaye alinifundisha,” anasema.

Fundi Nyata alianza kutengeneza mifuko na kuiuza kuanzia Sh1,500 hadi Sh3,500 kulingana na gharama ya utengenezaji kama muundo na kitambaa kilichotumiwa.

Wakati wa sherehe za muziki na maigizo, Fundi Nyata anaandika na kuuza michezo za kuigiza, aya za matumbawe na simulizi kwa shule tofauti.

Alipoulizwa jinsi anavyokabiliana na ushindani, Fundi Nyata anasema kwamba mifuko yake ni ya kipekee. Bidhaa zake huanzia, mkoba, begi za kusafiri, mifuko ya ununuzi wa bidhaa na viatu alivyojishonea mwenyewe.

“Ninatumia vitambaa vya aina tofauti; Ankara, makonge, hariri na Maasai shukas.Ningependa kuchanganya mtindo na taaluma yangu kama mwalimu kuliko kuacha mtindo kwani ni talanta yangu na inanipatia riziki za kila siku, “alisema.

Mkakati wake wa uuzaji ni hasa kupitia majukwaa ya kijamii .

Kustawi kwa biashara yake humpatia faida ya Sh 20,000 hadi Sh 50,000 kwa mwezi .Fundi Nyata anasema kuwa mashine za kutosha na kupata vyanzo vya vifaa bado ni changamoto kwake

Yeye anataka kufundisha watu zaidi juu ya kutengeneza mifuko Mzaliwa wa pili wa ndugu zake wanne anasema kwamba ana uwezo wa kuwasaidia familia yake kifedha kutokana na biashara yake.

You can share this post!

AKILIMALI: Jifunze biashara ya kurembesha viatu

AKILIMALI: ‘Ninaunda maelfu kutokana na...

adminleo