• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
RIZIKI: Ushonaji majaketi na makoti ya kupendeza wamvunia hela

RIZIKI: Ushonaji majaketi na makoti ya kupendeza wamvunia hela

Na MAGDALENE WANJA

PETER Okatch ni mshonaji nguo ambaye ujuzi wake umemwezesha kushona majaketi na makoti yenye ubora wa hali ya juu.

Ujuzi wake wa kipekee umemzolea umaarufu si tu miongoni mwa wateja wa kawaida, lakini pia na watu maarufu ambao hupendelea aina hizo za makoti majaketi.

Yeye kuanza kushona nguo hizi ni kutokana na msukumo uliochochewa na kifo cha kakake ambaye alipenda mavazi ya kuvutia. Aliamua kuanzisha kampuni ambayo ingehusika na ushonaji wa nguo za kupendeza kama kumbukumbu ya nduguye.

“Marehemu kakangu alipenda sana mavazi ya kupendeza na nilivutiwa sana na mavazi yake. Kama sehemu ya kumbukumbu yake, niliamua kuanzisha kampuni hii,” anasema Okatch.

Aliifungua kampuni kwa jina King Sidney.

Hi ni baada ya kupata shahada katika kozi ya Biashara na Uhasibu – Entrepreneurship and Accounting – katika Chuo Kikuu cha United States International University (USIU) mnamo mwaka 2016.

Okatch sasa anahusika na ushonaji wa makoti na majaketi ya kisasa ambayo hutengenezwa kwa kutumia vitambaa kutoka nchi mbalimbali.

“Kwa sasa kampuni hii inahusika na ushonaji wa makoti na majaketi pekee kwa sababu hizo ndizo aina za nguo nimebobea kushona,” anaongeza.

Idadi kubwa ya wateja wake ni wale walio na umri wa miaka 35 na kuendelea, japokuwa kuna idadi ndogo ya wateja wenye umri wa chini.

Koti moja anauza kwa bei ya kati ya Sh28,500 na Sh64,500 kutegemea aina na muundo.

Kupitia www.kingsidney.co.ke ameweza kuwafikia wateja wengi.

You can share this post!

Newcastle United kufungulia mifereji ya fedha kumsajili...

COVID-19: WHO yawataka watu waishi kwa tahadhari kuu jinsi...

adminleo