• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Safari Rally yasogezwa 2021 kwa sababu ya corona

Safari Rally yasogezwa 2021 kwa sababu ya corona

Na GEOFFREY ANENE

MASHABIKI wa mbio za kifahari za magari za Safari Rally nchini Kenya watasubiri hadi mwaka 2021 kushuhudia madereva wakishindania ubingwa wa taji hilo baada ya kuondolewa kwa duru hiyo Ijumaa kwenye ratiba ya Mbio za Magari za Dunia (WRC) mwaka 2020 kutokana na virusi hatari vya corona.

Wakenya walikuwa na hamu kubwa watapata kushuhudia mbio hizo zilizoratibiwa kurejea mwezi Julai 16-19 mwaka 2020 baada ya Kenya kupoteza hadhi ya dunia miaka 17 iliyopita.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa Serikali ya Kenya, Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (FIA) na WRC imesema Ijumaa kuwa athari za ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa uchumi, usafiri kutoka nchi moja hadi nyingine na masharti dhidi ya mikusanyiko zimechangia katika uamuzi huo kufanywa.

Duru hiyo ya Kenya inakuwa ya pili kwenye ratiba ya WRC kuondolewa mwaka 2020 kwa sababu ya virusi vya corona baada ya ile ya Ureno, na ya tatu baada ya duru ya Chile, ambayo ilifutiliwa mbali mwezi Novemba 2019 kutokana na hali ya wasiwasi ya kisiasa nchini Chile.

“Tutaendelea kujiandaa kwa Safari Rally kwa sababu tumepiga hatua kubwa na tunatumai kukaribisha madereva na maafisa mbalimbali wa mbio za magari na mashabiki mwaka ujao,” amesema Waziri wa Michezo Amina Mohamed.

Kenya inaendelea kushuhudia visa vya corona vikiongezeka. Vilifika 781 Ijumaa.

You can share this post!

COVID-19: Rais Kenyatta atarajiwa kutangaza hatima ya kafyu...

BURUDANI: Alikawia kujitosa kwa muziki kwa kudhania ulikuwa...

adminleo