SIHA NA LISHE: Matumizi mbalimbali ya majani ya mnaanaa yaani “mint leaves”
Na MARGARET MAINA
MAJANI ya mnaanaa – yaani majani ya mint plant – hupatikana sokoni na yana faida mbalimbali.
Hutibu maumivu ya mwili kwa ujumla.
Husaidia kuyeyusha chakula tumboni na kufanya mtu kupata choo chepesi.
Husaidia magonjwa wenye matatizo katika mfumo wa kupumua yaani respiratory disorders.
Husaidia kufifisha mkereko wa matumbo. Dalili za hali hii ni pamoja na msokoto wa tumbo, maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi, kukosa haja kubwa, kuharisha, nakadhalika
Husaidia kushusha shinikizo la juu la damu.
Husaidia kutibu maradhi na matatizo ya ngozi kama chunusi na kadhalika.
Husaidia kuboresha afya ya kinywa. Huua vijidudu vinavyosababisha matundu kwenye meno na pia huondoa harufu mbaya kinywani.
Husaidia kukabili kichefuchefu.
Pia majani haya husaidia kuboresha kumbukumbu.
Namna ya kutumia majani ya mnaanaa
Kwa matatizo yote yaliyotajwa isipokuwa maradhi na matatizo mbalimbali ya ngozi, kinywa, na kuboresha kumbukumbu, tumia chai iliyoandaliwa kwa majani ya majani ya mnaanaa. Kila siku chemsha kiasi cha kiganja kimoja cha majani ya mnaanaa kwenye vikombe viwili vya chai vya maji na unywe chai hiyo bila kuongeza sukari.
Kwa matatizo ya ngozi, kila siku pondaponda kiasi kiganja kimoja cha majani ya mnaanaa na ubandike mkorogo huo kwenye eneo lililoathirika kwa muda wa dakika 10 kisha uoshe.
Kwa afya ya kinywa kila siku chemsha kiganja kimoja cha majani ya mnaanaa kwenye vikombe viwili vya maji. Sukutua maji hayo mdomoni kwa muda wa dakika tano kisha uteme.
Unaweza pia kuchukua unga wa majani makavu ya mnaanaa na kupigia mswaki.