Jinsi unavyoweza kujitengenezea sabuni nyumbani
Na MARGARET MAINA
Muda wa kuandaaa: Dakika 30
Kiasi: Lita 25
Vinavyohitajika (Vitu hivi utavipata dukani kunakouzwa bidhaa za kutengenezea sabuni)
Maji lita 25
Kemikali ya Sulphonic
Manukato uyapendayo
Rangi (kijani/nyekundu au uipendayo)
Chumvi
Glycerin
Soda ash light
Formalin na alka.
Chombo chenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita 25
Maelekezo
Chukua sulphonic lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea (lita 25) kisha changanya na Slec.
Chukua soda ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita tano katika chombo kingine.
Ukishafanya hivyo, chukua mchanganyiko wako huo na umwagilie katika chombo chako chenye mchanganyiko wa sulphonic na Sles halafu mimina maji lita 15 na ukoroge kwa muda wa dakika 10.
Kisha weka rangi kiasi cha vijiko vitatu vya chai lakini angalia isizidi sana. Koroga tena vizuri.
Kisha chukua Glycerin vijiko viwili vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo chako.
Sasa ni wakati mwafaka wa kuweka kiasi unachotaka cha manukato yatakayofanya sabuni yako inukie vizuri.
Koroga chumvi pembeni; kiasi kidogo tu kama vijiko sita vya chai kisha mwagilia katika mchanganyiko wako na ongezea kiasi cha maji mpaka kufikia lita 25 .
TAHADHARI: Valia barakoa na glavu unapotengeneza sabuni hii na hakikisha unapata ushauri wa wataalamu wa kemikali na mamlaka za uhifadhi mazingira kama vile Nema nchini Kenya.