• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 6:45 PM
Cheruiyot aandikisha muda bora katika mbio za Maurie Plant zilizotawaliwa na ndugu watatu wa Norway

Cheruiyot aandikisha muda bora katika mbio za Maurie Plant zilizotawaliwa na ndugu watatu wa Norway

Na CHRIS ADUNGO

BINGWA wa dunia katika mbio za mita 1,500, Timothy Cheruiyot alisajili muda bora zaidi katika mbio za Maurie Plant Memorial zilizotawaliwa na ndugu watatu wa Ingebrigtsen kutoka Norway.

Mbio hizo za mita 2,000 ziliandaliwa sambamba katika uwanja wa Nyayo Nairobi na jijini Oslo Norway mnamo Juni 11, 2020.

Cheruiyot aliwaongoza Wakenya wenzake Elijah Manangoi, Edward Meli, Vincent Keter na Timothy Sein kutoana jasho na wapinzani wao Jakob, Filip na Henrik kutoka Norway.

Wanariadha hao wa Norway walichukua uongozi wa mbio hizo za Maurie kuanzia mwanzo hadi utepeni huku Jakob, 19, akiwaongoza nduguze kutawala nafasi tatu za kwanza.

Jakob Ingebrigtsen alisajili muda wa dakika 4:50 na kuivunja rekodi ya dakika 4:51.39 iliyowekwa na Mwingereza Steve Cram katika mbio hizo mnamo 1985.

Hicham Al-Guerrouj wa Morocco ndiye mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 1,500. Aliiweka rekodi hiyo ya muda wa dakika 4:44.79 mnamo 1999.

Ndugu wote watatu wa Norway walikamilisha mbio hizo chini ya muda wa dakika 4:57 huku Cheruiyot aliyesajili muda bora zaidi kwa upande wa wanariadha wa Kenya waliostahimili mvua na baridi kali, akifika utepeni baada ya muda wa dakika 5:03.05

Meli alimaliza mbio kwa muda wa dakika 5:13.02 huku Manangoi ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia, Jumuiya ya Madola na bara la Afrika katika mbio za mita 1,500 akiandikisha muda wa dakika 5:18.63

You can share this post!

Drama Abenny Jachinga akizikwa

Liverpoool wakubaliwa kuchezea mechi zao Anfield

adminleo