• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 12:15 PM
Madiwani wawili wang’olewa kamatini Bunge la Bungoma

Madiwani wawili wang’olewa kamatini Bunge la Bungoma

BRIAN OJAMAA

Masaibu yanayokumba utawala Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati yanaonekana yakiwa mbali kuisha baada ya madiwani kuwang’oa mamlakani wanachama wawili wa kamati ya mbunge la kaunti.

Mwanachama wa Kamati ya Afya na Usafi Antony Walela alitolewa na madiwani hao asubuhi huku mwenzake wa Usimamizi wa Umma Richard Sabwami Keya aking’atuliwa majioni kufuatia mjadala wenye hisia kali.

Madiwani 42 waliunga mkono kutolewa kwa wanachama hao wawili huku madiwani 9 wakipinga mjadala huo.

Mjadala huo ulikuwa umeongozwa na diwani wa Bukusu Sospeter Nyongesa. Bw Sabwami alikuwa analaumiwa kwa kutoajiri viongozi wa vijiji huku pesa zilizotengwa zikirudishwa kwenye hazina.

Kamati imeundwa ili kumchunguza na kurejesha majibu baada ya siku kumi. Madiwani 38 waliunga mkono kutolewa kwa Dkt Walela huku 13 wakipinga.

Mwada huo uliongozwa na diwani wa Lwandanyi,Tony Barasa aliyelaumu Dkt Walela kwa ufisadi na mapendeleo..

Bunge hilo lilimlaumu Dkt Walela kwa kuruhusu ufisadi kuendelea katika fedha zilizotengwa kushughulikia corona.

Alilaumiwakwa pia kukaa kimya wakati Sh 6.9 milioni zilitumiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bungoma kununua mitungi 600 kwa Sh10,000 kila mtungi.

Alilaumiwa kwa kumpa shemejiye tenda ya kusambaza vifaa vya Hospitali ya Bumula.

You can share this post!

Wauguzi wagoma kwa mara ya 4 mwaka huu Kisumu

Hofu watu wengi zaidi huenda wakaangamia kwa corona Afrika...

adminleo