• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:07 PM
West Ham waduwaza Chelsea na kuweka hai matumaini ya kutoshushwa ngazi

West Ham waduwaza Chelsea na kuweka hai matumaini ya kutoshushwa ngazi

Na CHRIS ADUNGO

BAO la dakika za mwisho kutoka kwa fowadi Andriy Yarmolenko liliwawezesha West Ham United kuzamisha chombo cha Chelsea kwa magoli 3-2 katika gozi la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Julai 1, 2020 uwanjani London.

Matokeo hayo yaliweka hai matumaini ya West Ham kuepuka shoka la kuwateremsha daraja katika kampeni za msimu huu.

Hasira za West Ham zilichochewa zaidi katika mechi hiyo baada ya bao la Tomas Soucek kutupiliwa mbali dakika chache kabla ya Chelsea kufungiwa penalti na Willian katika dakika ya 42.

Chini ya kocha David Moyes, West Ham walisawazishiwa na Soucek mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya Michail Antonio kuwaweka uongozini katika dakika ya 51.

Juhudi hizo za Antonio aliyedaiwa kuotea wakati Soucek alifumwa nyavu za Chelsea mara ya kwanza, zilifutiliwa mbali na Willian aliyesawazisha mambo katika dakika ya 78.

Ushirikiano mkubwa kati ya Antonio na Soucek lilichangia goli la tatu la West Ham ambalo lilijazwa kimiani na Yarmolenko katika dakika ya 89.

West Ham kwa sasa wanajiandaa kuchuana na Newcastle United ugenini kabla ya kuwaalika Burnley uwanjani London.

Ushindi katika mechi hizo huenda ukawaondoa katika hatari ya kushushwa ngazi kwa pamoja na Watford, Aston Villa, Bournemouth na Norwich City ambao kwa sasa wanakokota nanga kwa alama 21.

West Ham wanashikilia nafasi ya 16 jedwalini kwa alama 30, tatu pekee mbele ya Bournemouth na Villa.

Kushindwa kwa Chelsea ambao kwa sasa wanajiandaa kupepetana Watford mnamo Julai 4 uwanjani Stamford Bridge kunawaweka katika hatari ya kupitwa na Manchester United na Wolves na hivyo kukosa nafasi ya kushiriki kivumbi cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao.

Chelsea kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL kwa alama 54, mbili pekee mbele ya Man-United na Wolves watakaokuwa wenyeji wa Arsenal mnamo Julai 4 ugani Molineux.

  • Tags

You can share this post!

Wanne waliouawa na mama yao wazikwa

Wanafunzi kutoka Sudan wapimwa

adminleo