• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
Biashara ya vinyago inalipa

Biashara ya vinyago inalipa

NA RICHARD MAOSI

Muungano wa wauzaji na wachongaji wa vinyago kutoka soko la Maasai Market Nakuru wamekuwa wakichangia pakubwa katika pato la kaunti hususan kupitia njia ya utalii.

Baadhi yao wakiwa wamejiajiri na wengine kuajiriwa, mchakato mzima ukilenga kutengeneza nafasi nyingi za ajira miongoni mwa vijana kutoka mitaa duni ya Rhonda, Kivumbini, Bondeni, Freearea na Lanet.s

Lakini tangu janga la Covid -19 kubisha hali yapata miezi mitatu iliyopita, sekta ya utalii ilipata pigo kubwa huku safari za watalii wanaoingia na kutoka humu nchini zikipigwa marufuku.

Pia serikali ilifunga mipaka na kubana malango ya kuingia katika mbuga maarufu za wanyama wa porini katika juhudi za kuzuia msongamano wa watu .

Ni kwa sababu hiyo wachongaji vinyago wanakadiria hasara kubwa, huku hazina yao ya vinyago ikibakia kwenye sefu bila ya wanunuzi waliokuwa wamezoeleka kutembelea mabanda yao, kujionea na kuchukua bidhaa.

“Misimu ya Pasaka, wikendi na Sikuu za kitaifa zikikuwa ni baadhi ya siku zilizokuwa zikivutia idadi kubwa ya wageni,”asema Evans Nyabwage katika mahojiano maalum na Taifa Lida ya Zaidi ya 200eo Dijitali.

Evans alianzisha kazi ya kuuza vinyago mwaka wa 1996 kwa mtaji wa 500, ana ujuzi wa zaidi ya mwongo mmoja kazi anayoichukulia kama nyingine ile muradi mtu awe mwenye bidii.

Alitumia wakati wake mwingi kuwafundisha wanawe ujuzi wa kazi hii akiamini kuwa siku moja wangekuja kuridhi mikoba yake ili waendeleze taaluma.

Kulingana naye wanunuzi wengi ni watalii wanaotembelea mbuga zinazopatikana katika sehemu za Bonde la Ufa , maeneo ambayo hupakana na kaunti ya Nakuru kwa mfano ziwa Baringo,Thompson Falls na Lake Nakuru National Park.

Mara nyingi kabla ya Corona kuingia mauzo yalikuwa ni mazuri na kazi yenyewe imemsaidia kununua kipande cha ardhi na kuwasomesha watoto wake hadi kiwngo cha Chuo Kikuu.

Alieleza kuwa mawe ya kuchonga vinyago yana upekee wake na mara nyingi hutoka katika kaunti ya Kisii, yawe magumu na laini sawia muradi yasije yakatengeneza nyufa wakati wa kulainisha.

Mawe haya yanayofahamika kama soap Stone, yana sifa sifa maalum kwani hayawezi kutengeneza nyufa wala kuchakaa.Ingawa ni nadra kupatikana isipokuwa katika maeneo fulani nchini kama vile Nyanza na mkoa wa Magharibi.

Evans aliongezea kuwa ni lazima mchongaji vinyago aelewa mahitaji ya wanunuzi na kutengeneza bidhaa zinazoendana na wakati ili asije akapitwa na wakati katika mfumo huu wa utandawazi.

Ajibidiishe kutangeneza uwanda mpana wa soko la humu nchini na lile la kimataifa kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Watsaap.

Evans anasema yeye hutengeneza kila aina ya bidhaa kuanzia shanga, mikufu, bangili na kushona mavazi ya kiasili, shati zenye nembo ya bendera ya taifa, na mikufu ya thamani akitumia ngozi za wanyama.

Ambapo wanunuzi wake ni wa majira, nyingi ya bidhaa zake akiuza katika soko wazi la Maasai Market katikati ya mji wa Nakuru, mara nyingine mtandao wa kijamii umekuwa ukimfikisha katika soko la Kitaifa ambapo uagizaji umenoga.

 ingawa msimu huu wa Corona idadi ya wanunuzi imeshuka jambo linalomlazimu wakati mwingine kutembeza bidhaa zake katika makazi rasmi ya watu.

“Kwa ujumla mapato yameshuka na soko letu limekuwa finyu, mara nyingi tunalazimika kuuza mikufu kwa bei ya kutupa ili kujaza kodi ya kulipia nyumba ya kufanya biashara,”akasema.

Awali alikuwa akitengeneza faida ya Zaidi ya 2000 kwa siku huku bidhaa zake nyingi zikiwa ni kati ya 500-2000.

Anasema kuwa endapo mjasiria mali atajizatiti kazini mwake anaweza kutengeneza zaida ya 50,000 ila mwezi kama faida tu, hii ni baada ya kuondoa ad azote za matumizi kama vile kulipia kodi na hela za vibarua wanaomsaidia wakati wa kutengeneza vyombo vyake.

Siku za mbeleni Evans analenga kuboresha huduma zake na kuingilia vitengo vya burudani na ulimwende ili kupanua soko la wanunuzi wake, ingawa atahitaji mtaji wa ziada.

Wito wake anaombaserikali kupunguza kodi inayotoza wakati wa kuanzisha biashara kama hii ili kuwawezesha vijana wengi wasiokuwa na ajira.

Aidha anapendekeza serikali kutengeneza taasisi mbalimbali ambazo zitawawezesha vijana kupata ujuzi na ufundi wa kutengeneza curios kwa kuwapiga msasa na kuwapatia mtaji kwa njia ya mkopo usiokuwa na riba.

Evans anawahimiza vijana kujiajiri badala ya kutegemea kazi za kuajiriwa kwa sababu mtu anaweza kujisimamia , ambapo nia yake ni kufikisha nembo katika soko za kimataifa na kuwaajiri vijana.

You can share this post!

Teknolojia inavyowasaidia chipukizi kufanya mazoezi

JOYCE OTIENO: Ielewe biashara ya uanamitindo

adminleo