• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:50 AM
Corona yazima ndoto za wachezaji

Corona yazima ndoto za wachezaji

NA JOHN KIMWERE

MWENYEKITI wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Tawi la Nairobi Magharibi, Hussein Bashir amesema hali sio hali tena katika sekta ya spoti baada ya mlipu ko wa virusi hatari vya corona kutisha shughuli zote.

Janga hilo lililotua nchini mwezi Machi mwaka huu linazidi kutesa wengi.. Hali hiyo imechangia njaa kwa wanaspoti wengi maana hawana mapato kuanzia kwa wachezaji, viongozi wao bila kuweka katika kaburi la waamuzi.

”Kusema kweli ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu imepitia baada ya adui huyo kushuka nchini nimezungumza na zaidi ya wamiliki wa klabu sita ambao wamefunguka kuwa wanaona giza mbele yao kisa na maana:corona,” Bashir alisema na kuongeza kwamba mlipuko huo umevuruga shughuli nyingi kufikia biashara za wadhamini wa klabu nyingi.

”Buda kubaya msoto balaa. Wamiliki hao wamesema kuwa kwanza watalazimika kuvunja timu zao watulia kwa muda wa msimu mmoja au mihula miwili maana hawaamini kama watapata ufadhili,” mwenyekiti akasema. Alidokeza kuwa klabu kadhaa za Ligi ya Taifa Daraja la Pili huenda hazitakuwapo kwenye kampeni za muhula ujao.

Katika mpango mzima endapo baadhi ya vikosi vya ngarambe hiyo huenda vitakosa udhamini sembuse timu za vipute vya Regional League na Ligi za Kaunti?

Naye kocha, Allan Shibega wa Kangemi Patriots anasema “Tunaomba serikali kupitia Wizara ya michezo ianze kuweka mikakati ya kuzipiga jeki timu za michezo mbali mbali nchini ambazo hushiriki ligi za chini.”

Akipiga soga na Mwanaspoti aliweka wazi kuwa itakuwa vigumu kwa baadhi ya klabu za mchezo huo kupata ufadhili kisa na maana uchumi umeporomoka kwa kiwango kikubwa nchini.

Kadhalika anasema ingawa wachezaji wake huwa wanashiriki mazoezi ya kibinafsi manyumbani mwao hana uhakika endapo bosi wao atakuwa katika hali nzuri kifedha kugharamia shughuli za kikosi hicho kwenye kampeni za msimu ujao.

Hakika janga la corona lilishuka nchini muda mchache baada ya zaidi ya wanasoka 1000 kuanza kuwaza na kuwazua wakisaka pa kuelekea.

Ni wachana nyavu wa klabu 32 za kipute cha Super Eight Premier League (S8PL) na Ligi ya Daraja la Kwanza. Hii ni baada ya mapema mwaka huu kampuni ya Extreme Sports kutangaza kuwa haitoweza kuandaa mechi za ligi zake mbili msimu uliyositishwa na corona kwa kukosa ufadhili. Ni tangazo lililotolewa na Athanas Obango ambaye amekuwa mshirikishi wa michezo hiyo linaloendelea kuwaumiza wengi.

You can share this post!

Motisha baada ya KWPL kutengewa Sh14 bilioni

Mchuuza maji sasa amiliki chuo cha urembo

adminleo