• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:23 PM
Ngelel na Mukhwana washindwa kutetea mataji Dalian Marathon

Ngelel na Mukhwana washindwa kutetea mataji Dalian Marathon

Na GEOFFREY ANENE

MABINGWA wa Dalian Marathon mwaka 2017, Willy Ngelel na Ednah Mukhwana wamepoteza mataji yao kwa wakimbiaji Edwin Kibet Koech na Mulu Seboka nchini Uchina, Jumapili.

Koech amekuwa mkimbiaji wa kwanza katika historia ya Dalian Marathon kutimka chini ya saa 2:10 baada ya kutwaa taji kwa saa 2:09:44.

Mkenya huyu mwenye umri wa miaka 30, ambaye muda wake bora ni 2:08:17 alioweka mjini Eindhoven nchini Uholanzi miaka mitatu iliyopita, alimzidi kasi Ngelel katika kilomita sita za mwisho na kuvunja rekodi ya Dalian Marathon ya saa 2:13:03 iliyowekwa na Mkenya Julius Maisei mwaka 2012.

Mkenya Ngelel aliandikisha muda wake bora alipokamilisha nyuma ya Koech kwa saa 2:10:31 naye Muethiopia Habtamu Wegi akafunga tatu-bora (2:12:17).

Muethopia Mulu Seboka alivumilia maumivu ya tumbo na kutwaa taji la wanawake kwa saa 2:28:59. Wakenya Mukhwana na Rodah Jepkorir waliridhika katika nafasi mbili zilizofuata kwa saa 2:32:06 na 2:32:53, mtawalia.

You can share this post!

Gor yalemewa na Hull City kwa penalti licha ya Oluoch...

Mabao 31 yavumwa siku ya mwisho ya EPL, Salah avunja rekodi

adminleo