• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:03 PM
LISHE: Keki ya ‘pundamilia’

LISHE: Keki ya ‘pundamilia’

Na MISHI GONGO

Idadi ya walaji: 8

Viungo

unga wa keki (self-rising) gramu 500

sukari gramu 300

mayai 5

siagi gramu 300

rangi ya poda (iwe ya waridi)

Jinsi ya kutayarisha

Changanya sukari, siagi na kiasi cha aiskrimu ndani ya bakuli kisha kwa kutumia mwiko au mchapo, changanya hadi vilainike.

Ongeza mayai yako endelea kukoroga hadi vichanganyike vizuri.

Ongeza unga kidogo kidogo katika mchanganyiko wako hadi mchanganyiko uwe mzito.

Gawanya mchanganyiko wako mara mbili kwa bakuli moja; tia rangi ya poda na mchanganyiko uliosalia uache jinsi ulivyo.

Chukua mkebe wako wa kuoka upake siagi ili kuzuia keki yako kuganda mkebeni

Mimina mchanganyiko wa rangi ya poda kwa mkebe utengeze uwa mstari. Fuatisha na mchanganyiko usio na rangi hadi mchanganyiko wako umalizike.

Oka kwa dakika 60 ukitumia moto wa nyuzi 200

Subiri upoe kisha kwa taratibu, utoe kwenye mkebe kisha andaa.

Unaweza kula huku ukinywa ama chai au sharubati.

You can share this post!

Rais akiuka ahadi ya kutii sheria

Kisumu All Stars sokoni kutafuta kocha mpya na maafisa wa...