• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
Tencent Sports kupeperusha mechi za EPL nchini China

Tencent Sports kupeperusha mechi za EPL nchini China

Na MASHIRIKA

VINARA wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wameafikiana na China kuhusu mpango wa kupeperusha mechi zote zilizosalia katika kampeni za msimu huu wa 2020-21.

EPL imetia saini mkataba na kampuni ya Tencent Sports baada ya kandarasi yake ya awali ya Sh81 bilioni na PPTV kutamatishwa mara moja mwanzoni mwa Septemba 2020.

Mashabiki wa soka ya EPL sasa nchini China watakuwa na fursa ya kufuatilia michuano ya kivumbi moja kwa moja kwenye runinga zao kuanzia wikendi hii.

Makubaliano ya awali kati ya EPL na PPTV yalitiwa saini mnamo 2019 na yalikuwa yakatike rasmi mnamo 2022 baada ya salio la Sh22 bilioni kutolipwa kufikia Machi 2020.

China imekuwa mojawapo ya nchi ambazo zimekuwa zikiingia katika dili za fedha nyingi na EPL kwa minajili ya kupeperusha mechi za kivumbi hicho nje ya bara Ulaya.

Magazeti mengi nchini Uingereza na China yameripoti kwamba kiini cha kuvunjika kwa uhusiano kati ya EPL na PPTV ni za kifedha wala si za kisiasa.

Zaidi ya nusu ya mechi 372 zilizosalia katika EPL msimu huu sasa zitatazamwa bila malipo yoyote na mashabiki wa soka ya China huku nyinginezo zikihitaji mashabiki kujisajilisha ndipo wafurahie uhondo wa michuano yenyewe.

Kwa mara ya kwanza, klabu zitakubaliwa pia kutumia mashabiki video fupi za baadhi ya mechi zao huku wanasoka wakiruhusiwa kutangamana moja kwa moja na mashabiki kupitia mpango huo. Hayo yamethibitishwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa EPL, Richard Masters.

TAFSIRI: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Messi azamisha chombo cha Girona

Mechi za FKF Shield kurejelewa