• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 12:30 PM
Eymael akaribia kuingia K’Ogalo

Eymael akaribia kuingia K’Ogalo

Na JOHN ASHIHUNDU

Aliyekuwa kocha wa Yanga, Luc Eymael anakaribia kuajiriwa na Gor Mahia kwa ajili ya msimu ujao.

Gor Mahia kwa sasa hawana kocha mkuu baada ya Steven Polack kuondoka nchini kuelekea Finland na kuiacha timu hiyo katika hali ya utatanishi, licha ya kuahidi kurejea kabla ya msimu mpya kuanza.

Eymael amekuwa hana kazi tangu atimuliwe na Yanga mwishoni mwa msimu wa 2019/20, baada ya kufokeana na mashabiki waliomshutumu kwa kushinda kutwaa taji lolote.

Kocha huyo mwenye umri wa 61 ambaye kwa sasa yuko nchini kwao Ubelgiji amefichua kwamba Gor Mahia wamemfikia wakitaka asini mkataba wa kuchugua kazi hiyo.

“Gor Mahia wametuma maombi yao wakitaka niwe kocha wao, lakini sijaamua,” Eymael alithibitisha habari hizo jana.

“Iwapo tutaelewana, niko tayari kuanza kazi, kumbuka hakuna kocha nchini Kenya anayeweza kufikia mataji yangu (sita kwa jumla), nakumbuka wamefuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika na bila shaka wako na pajeti, ingawa hatujaelwana. Nimewapa barua zangu na walisema watafikiria kuhusu jambo hilo.”

Alioulizwa kinachomfanya afurahie moambi ya Gor Mahia, Eymael alisema: “Niko tayari kwa sababu sina kazi kwa sasa. Nilikuwa na Yanga lakini hawakutimiza masharti yangu nilivyotaka.”

Eymael aliongeza: “Nadhani nimeimarika zaidi, na ningependa nifanya kazi nchini Kenya kwa mara ya pil. Niko tayari kujiunga na timu yoyote, na hayo ndio malengo yangu.”

Polack, aliyejiunga na Gor Mahia mwanzoni mwa msimu uliopita kuchukuwa nafasi ya Hassan Oktay, alipewa likizo ya siku 10 kutembelea familia yake nyumbani.

Wakati huo huo, katibu mkuu wa klabu hiyo, Samuel Ocholla amekanusha madai kwamba wamefanya mazungmzo na kocha wao wa zamani Ze Maria kurejea klabuni.

Eymael, ambaye amenoa timu tofauti nchini Afrika Kusini, Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pia aliwahi kuandaa AFC Leopards ambao ni wapinzani wakuu wa Gor Mahia.

  • Tags

You can share this post!

Mechi za FKF Shield kurejelewa

Fowadi ‘Crucial’ Wasambo kurejea KPL