• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Beki wa Hamburg nchini Ujerumani aadhibiwa vikali

Beki wa Hamburg nchini Ujerumani aadhibiwa vikali

Na MASHIRIKA

BEKI Toni Leistner wa Hamburg nchini Ujerumani, amepigwa marufuku ya mechi tano na kutozwa faini ya Sh1 milioni kwa hatia ya kumpiga shabiki aliyemrushia cheche za matusi wakati wa mechi ya German Cup iliyowakutanisha na Dynamo Dresden.

Dresden waliibuka washindi wa gozi hilo la Septemba 18, 2020 kwa mabao 4-1.

Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) limesema kwamba Leistner, 30, “alitusiwa mara nyingi na shabiki wa kikosi cha Dresden kabla ya sogora huyo kupandwa na hasira na kuamua kumvamia na kutandika makofi kadhaa.”

Japo alichokozwa, DFB limeshikilia kwamba Leistner alivunja kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona na alihatarisha maisha yake kwa hatua ya kumvamia shabiki huyo “mtundu”.

“Kutokana na kitendo chake, alihatarisha maisha yake. Pia alimweka shabiki huyo katika hatari ya kuambukizwa au kuumia,” ikasema sehemu ya taarifa ya DFB.

Takriban mashabiki 10,000 walihudhuria mchuano huo kati ya Hamburg na Dresden. Idadi hiyo ilikuwa ya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa uwanjani tangu kurejelewa kwa soka ya Ujerumani baada ya kulegezwa kwa baadhi ya kanuni zinazodhibiti msambao wa ugonjwa wa Covid-19.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mfumaji Diogo Jota atua Liverpool kwa Sh5.7 bilioni

Aguero kusalia nje kwa miezi miwili zaidi kuuguza jeraha la...