• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 12:58 PM
Arsenal wamsajili kipa Runnarsson kuwa kizibo cha Martinez

Arsenal wamsajili kipa Runnarsson kuwa kizibo cha Martinez

Na MASHIRIKA

ARSENAL wamejinasia huduma za kipa raia wa Iceland Runar Alex Runarsson ambaye ametia saini mkataba wa miaka minne kutoka kambini mwa Dijon nchini Ufaransa.

Runnarsson, 25, amesajiliwa na Arsenal ili awe kipa chaguo la pili baada ya kuondoka kwa Emiliano Martinez aliyeyoyomea Aston Villa na kumwacha Bernd Leno ambaye amekuwa akitegemewa pakubwa na kocha Mikel Arteta.

Runnarsson alijiunga na Dijon ya Ligu Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Julai 2018 na akawajibishwa na kikosi

“Nimefurahi sana kutia saini mkataba wa muda mrefu na Arsenal. Hizi ni habari njema kwangu na familia yangu nzima,” akatanguliza Runnarsson.

“Najua ninasubiriwa na kibarua kigumu ugani Emirates, lakini nitajitahidi kujituma kwa kadri ya uwezo wangu ili nijivunia muda wa kutosha wa kuwadakia Arsenal,” akasema.

Kocha Mikel Arteta wa Arsenal alisema: “Tunataka kuleta ushindani usiokuwa na msuguano wowote usiostahili uwanjani Emirates. Naamini kwamba ujio wa Runnarsson utaimarisha zaidi uthabiti wa idara hiyo.”

You can share this post!

Maraga ashauri Uhuru kuvunja Bunge la Kitaifa

Sogora mwingine wa Wazito FC astaafu na kupokezwa majukumu...