• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 7:55 AM
Wavumbua mashine inayoua virusi vya corona kwenye vifaa

Wavumbua mashine inayoua virusi vya corona kwenye vifaa

By Kevin Rotich

[email protected]

Janga la corona limetatiza hali ya kawaida ya maisha kuanzia kwenye sekta za burudani, hoteli, muziki, uchuuzi na pia usafiri wa ndege.

Kwa sasa ni vigumu kwa mtu kuingia kwenye mkahawa, maeneo ya umma ama benki na kufanya ununuzi akitumia hela.

Ni kutokana na changamoto hizo ampapo Dominic Gichuma na Juma Phelix walivumbua mashine kwa jina Taa Sterilizer ambayo inaweza kuua virusi vya corona.

Taa Sterilizer, ambayo inatumia teknolojia ya Ultra Violet Germicidal Irradiation (UVGI), ni kifaa ambacho kinaua virusi na bakteria kwenye vifaa kupitia makali ya mwangaza.

“Wakati SARs-CoV-2 thymine (ambayo ni mojawapo ya necleobasi inayopatika katika chembechembe za DNA ya korona) inapopatana na mwenge wa UVGI, inaua mojawapo ya kiungo muhimu cha virus vya corona na kumaliza makali,” anasema Bw Gachuma.

Uvumbuzi wao ulipigwa jeki na rais Uhuru Kenyatta mwezi wa Juni aliposihi sekta zote kupunguza utumiaji wa pesa za shilingi au noti ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa corona.

“Mwezi wa Aprili, wakati visa vya corona vilipokuwa vikipanda, nilizungumza na Bw Phelix, kijana wa miaka 26 ili tuweze kuunda kifaa hiki kabla ya kupata ruhusa kutoka kwa Kenya Nuclear Regulatory Authority (KNRA) na shirika la kutathmini ubora wa bidhaa (KEBS,” Bw Gachuma, mwenye miaka 28, anaeleza.

Wakati huo, walikuwa wakiangalia iwapo mtambo huo unaweza kufanya kazi hiyo na usalama wake ukapongezwa na shirika la kimataifa Recommended Exposure Limits (REL).

Kwa sasa wamewaajiri watu watano na watarajia kuajiri watu wengine mia moja watakapoanza kutengeza vifaa hivyo kwa wingi. PICHA/ KEVIN ROTICH

“Mwezi wa Juni 21, tulipokea ripoti ya ukaguzi wa mashine na ruhusa kutoka kwa Kenya Medical Research Institute (KEMRI),” Bw Gachuma ambaye alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya anasimulia.

Baadaye, Julai 22, walipata ruhusa kutoka kwa mashirika ya KNRA and KEBS kuunda na kusambaza mashine hiyo.

Anasema waliwekeza kima cha Sh200,000 kwenye mradi huo kutoka kwa akiba yao. Vifaa hivyo vinalenga mashirika ya serikali na kibinafsi.

“Mashine hii inaua virusi ama bakteria kwenye noti, simu, kitufe, mswaki, vitabu, kalamu, vifaa vya ofisini, vifaa vya kujikinga na korona,  karatasina vifaa vya hospitali,” anasema.

Hata hivyo, anasema wanaweza kutengeza vifaa hivyo kwa maagizo wanayopokea ili kupunguza gharama ya kutengeza vifaa hivyo na kudhibiti viwango vya uzalishaji.

“Kwa sasa, tunavyo vifaa vinne ambavyo tunatumia hasa katika maonyesho kwa wateja wetu watarajiwa,” anaongeza.

Lakini anasema wamepokea maagizo ya kusambaza kutoka kwa mashirika kadhaa ambayo yanahitaji mashini hiyo.

“Tunajadiliana na kaunti ya Kiambu, na pia tumetuma barua kwa ofisi za serikali kwani kifaa hiki ni cha kwanza katika bara la Afrika kuvumbuliwa. Tunatumai tutapata majibu ya kuridhisha,” ananena.

Wanatarajia kutengeza mashini hizo kwa wingi. “Ili kufanikiwa, tunaitaji pesa nyingi ili tuweze kujumuisha opereshni zote ambazo zitapelekea kupungua kwa mahitaji ya kiwango hiki,” asema.

Kwa sasa wamewaajiri watu watano na watarajia kuajiri watu wengine mia moja watakapoanza kutengeza vifaa hivyo kwa wingi.

“Kiwango chetu cha kutengeza bidhha kwa mwezi michache inakayokuja (kulingana na maagizo) itakua 1000 kwa masaa 24 (mia tano mchana na 500 nyingine wakati wa usiku). Lakini, uzalishaji utakuwa sambamba kulingana na mahitaji na uzalishaji” anasema.

Anawasihi vijana wakubali kufanya kazi yeyote na wasikubali masomo waliyoyafanya kwenye vyuo vikuu na taasisi za kiufundi kutatiza harakati zao.

Pia anasema serikali inafaa kuwekeza kwenye makampuni ambayo yatachangia ukuuaji wa mashirika ya nyumbni na pia kuunga mkono vifaa vya nyumbai na sevesi.

“Tunapoagiza kila kitu kutoka mataifa ya ughaibuni, pesa izo zinarejea mataifa hayo lakini tukiunga zetu mkono peas hayo yatabaki humu na kuendeleza uchumi,” anasema.

You can share this post!

Arsenal waiondoa Leicester City kwenye Carabao Cup

Mafuriko yalivyotatiza wakulima Perkerra