• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Kibagare Slums yahitaji kupigwa jeki kuimarisha soka yake

Kibagare Slums yahitaji kupigwa jeki kuimarisha soka yake

Na JOHN KIMWERE 
KLABU ya Kibagare Slums ni kati ya timu zinazopania kujituma kiume kwenye kampeni za Ligi ya Kaunti ya Nairobi Magharibi muhula ujao. Timu hii iliozaliwa miaka 15 iliyopita inapatikana katika kijiji cha Kibagare karibu na mtaa wa kifahari wa Kitsuru Kaunti ya Nairobi.
Wanasoka wake hufanyia mazoezi Bamboo Stadium karibu na Shule ya Msingi ya St Martins.
 
CORONA
Shughuli za spoti zilipigwa breki tangia mwezi Machi 2020 pale janga la virusi hatari vya corona kutua nchini. ”Corona imepiga stopu shughuli za michezo ambapo tunahisi wachezaji wengi watapoteza makali yao tutakaporejea Viwanjani kwa ajili ya kushiriki mechi za ligi msimu ujao,” mwenyekiti wake Itotia Karanja.
Bosi huyo anaongeza kuwa wanataka kujitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha wanaibuka kati ya nafasi mbili bora na kuzoa tiketi ya kupandishwa ngazi kushiriki kipute cha Nairobi West Regional League (NWRL).
 
NAMBARI MBILI
Anadokeza kuwa wameshiriki ligi ya Kaunti kwa misimu mitano ambapo tayari sasa raundi hii hawana la ziada bali itawabidi wapambane mwanzo mwisho ili kutimiza azimio hilo. Ndani ya kipindi hicho inajivunia kumaliza nambari mbili kwenye mechi za ngarambe ya mwaka 2014.
”Licha ya changamoto za kukosa ufadhili tunaamini tuna wachezaji wazuri ambapo tukipigwa jeki tu ndani ya misimu miwili tu bila kujisifia tutafanya vizuri na kusonga mbele kushiriki ligi ya juu,” anasema kocha wake Johnstone Etale ambaye husaidiana na Simon Kimeu.
Hata hivyo anatoa mwito kwa viongozi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) wazamie mpango wa kutafuta wafadhili kusaidia timu za mashinani kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi.
 
BNSL
Katika mpango mzima meneja wake, Christopher Njenga anasema ndani ya miaka mitano ijayo wanadhamiria kuwa wakishiriki mechi za Betika Supa Ligi ya Taifa (BNSL) kupigania kufuzu kwa Ligi Kuu ya Kenya (KPL).
Ukosefu wa ufadhili unachangia Kibagare kushindwa kugharamia mahitaji ya kuendesha shughuli zao michezoni.
Kibagare ambayo mechi za ligi huchezea Uwanjani Kihumbu-ini Kangemi tangia ianzishwe mwaka 2015 inajivunia kulea wachezaji kadhaa waliokwenda kwingine akiwamo Amstone Agama(Gogo Boys).
Kibagare Slums FC inajumuisha wachana nyavu kama Jackson Aletia, Cetrick Isichi, Francis Thiong’o, Daniel Wakwaya, Emmanuel Mwangi, Dennis Njoroge, Moses Okili, Rodriguez Saitoti, Kevin Juma, Ibrahim Mise na Joshua Muthengi.
Pia wapo George Waithaka, Jive Kasyoki, Dennis Inoi, George Njenga (nahodha msaidizi), Eric Mumo (nahodha), Benson Mwangi, Kelvin Mukhovi na Alex Nyoga (nahodha msaidizi) bila kusahau Benson Otieno (katibu).
  • Tags

You can share this post!

IRENE NZUKI: Ndoto yangu ya kuwa mwigizaji itatimia

WINNIE MACHARIA: Nina mpango wa kuwasaidia waigizaji...